Lakini Mungu huwakokota wenye nguvu kwa uwezo wake;
ingawa wamestawi, hawana hakika ya maisha.
Aweza akawaacha wakapumzika wakijihisi salama,
lakini macho yake yanaona njia zao.
Kwa kitambo kidogo hutukuka,
hatimaye hutoweka;
hushushwa na kukusanywa
kama wengine wote;
hukatwa kama masuke ya nafaka.