“Hili ndilo agano nitakalofanya na nyumba ya Israeli
baada ya siku zile,” asema Mwenyezi Mungu.
“Nitaweka sheria yangu katika nia zao,
na kuiandika mioyoni mwao.
Nitakuwa Mungu wao,
nao watakuwa watu wangu.
Mtu hatamfundisha tena jirani yake,
wala mtu kumfundisha ndugu yake, akisema,
‘Mjue Mwenyezi Mungu,’
kwa sababu wote watanijua mimi,
kuanzia aliye mdogo hata aliye mkubwa kuliko wote,”
asema Mwenyezi Mungu.
“Nitasamehe uovu wao, wala sitazikumbuka dhambi zao tena.”