Mnapindua mambo juu chini,
kana kwamba mfinyanzi aweza kufikiriwa kuwa kama udongo wa mfinyanzi!
Je, kile kilichofinyangwa
chaweza kumwambia yule aliyekifinyanga,
“Wewe hukunifinyanga mimi”?
Je, chungu kinaweza kumwambia mfinyanzi,
“Wewe hujui chochote”?