1
Isaya 11:2-3
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Roho wa Mwenyezi Mungu atakaa juu yake, Roho wa hekima na wa ufahamu, Roho wa shauri na wa uweza, Roho wa maarifa na wa kumcha Mwenyezi Mungu naye atafurahia kumcha Mwenyezi Mungu.
Linganisha
Chunguza Isaya 11:2-3
2
Isaya 11:1
Chipukizi litatokea kutoka shina la Yese, kutoka mizizi yake Tawi litazaa tunda.
Chunguza Isaya 11:1
3
Isaya 11:4
bali kwa uadilifu atahukumu wahitaji, kwa haki ataamua wanyenyekevu wa dunia. Ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, kwa pumzi ya midomo yake atawaua waovu.
Chunguza Isaya 11:4
4
Isaya 11:5
Haki itakuwa mkanda wake na uaminifu utakuwa mshipi kiunoni mwake.
Chunguza Isaya 11:5
5
Isaya 11:9
Hawatadhuru wala kuharibu juu ya mlima wangu mtakatifu wote, kwa kuwa dunia itajawa na kumjua Mwenyezi Mungu kama maji yajazavyo bahari.
Chunguza Isaya 11:9
6
Isaya 11:6
Mbwa-mwitu ataishi pamoja na mwana-kondoo, naye chui atalala pamoja na mbuzi, ndama, mwana simba na ng’ombe wa mwaka mmoja watakaa pamoja, naye mtoto mdogo atawaongoza.
Chunguza Isaya 11:6
7
Isaya 11:10
Katika siku hiyo, Shina la Yese atasimama kama bendera kwa ajili ya mataifa. Mataifa yatakusanyika kwake, na mahali pake pa kupumzikia patakuwa utukufu.
Chunguza Isaya 11:10
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video