“Utawaamuru Waisraeli wakuletee mafuta safi ya zeituni yaliyokamuliwa kwa ajili ya mwanga ili zile taa ziwake mfululizo. Katika Hema la Kukutania, nje ya pazia lililo mbele ya Sanduku la Ushuhuda, Haruni na wanawe watahakikisha kuwa taa hizo zinawaka kuanzia jioni hadi asubuhi mbele za Mwenyezi Mungu. Hili litakuwa agizo la milele miongoni mwa Waisraeli kwa vizazi vijavyo.