Wafundishe hukumu na sheria zake, na uwaoneshe jinsi wanavyopaswa kuishi, na jinsi wanavyopaswa kuenenda. Lakini uchague watu wenye uwezo miongoni mwa watu wote, watu wanaomwogopa Mungu, watu waaminifu wanaochukia mali ya dhuluma, uwateuwe wawe maafisa juu ya maelfu, mamia, hamsini na makumi.