Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, anayewatangulia, atawapigania, kama alivyofanya kwa ajili yenu huko Misri, mbele ya macho yenu hasa, na pia huko jangwani. Huko mliona jinsi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, alivyowachukua, kama baba amchukuavyo mwanawe, katika njia yote mliyoiendea hadi mkafika mahali hapa.”