1
Matendo 20:35
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Katika kila jambo nimewaonesha kwamba kwa njia hii ya kufanya kazi kwa bidii imetupasa kuwasaidia wadhaifu, mkikumbuka maneno ya Bwana Isa mwenyewe jinsi alivyosema, ‘Ni heri kutoa kuliko kupokea.’ ”
Linganisha
Chunguza Matendo 20:35
2
Matendo 20:24
Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa ya thamani kwangu, kama kuyamaliza mashindano na kukamilisha ile kazi Bwana Isa aliyonipa, yaani kazi ya kuishuhudia Injili ya neema ya Mungu.
Chunguza Matendo 20:24
3
Matendo 20:28
Jilindeni nafsi zenu na mlilinde lile kundi lote ambalo Roho wa Mungu amewaweka ninyi kuwa waangalizi wake. Chungeni jumuiya ya waumini ya Mungu, aliowanunua kwa damu yake mwenyewe.
Chunguza Matendo 20:28
4
Matendo 20:32
“Sasa nawakabidhi kwa Mungu na kwa neno la neema yake, linaloweza kuwajenga na kuwapa ninyi urithi miongoni mwa wote ambao wametakaswa.
Chunguza Matendo 20:32
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video