1
2 Wakorintho 1:3-4
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Isa Al-Masihi, Baba wa huruma na Mungu wa faraja yote. Yeye hutufariji katika taabu zetu, ili tuweze kuwafariji walio katika taabu yoyote kwa faraja ambayo sisi wenyewe tumepokea kutoka kwa Mungu.
Linganisha
Chunguza 2 Wakorintho 1:3-4
2
2 Wakorintho 1:5
Kama vile mateso ya Al-Masihi yanavyozidi maishani mwetu, hivyo ndivyo faraja yetu inavyofurika kupitia kwa Al-Masihi.
Chunguza 2 Wakorintho 1:5
3
2 Wakorintho 1:9
Kwa kweli, mioyoni mwetu tulihisi tumekabiliwa na hukumu ya kifo, ili tusijitegemee sisi wenyewe bali tumtegemee Mungu afufuaye wafu.
Chunguza 2 Wakorintho 1:9
4
2 Wakorintho 1:21-22
Basi ni Mungu atufanyaye sisi pamoja nanyi kusimama imara katika Al-Masihi. Alitupaka mafuta kwa kututia muhuri wake na kutupatia Roho wake Mtakatifu mioyoni mwetu kuwa rehani kwa ajili ya kututhibitishia yote aliyotuahidi.
Chunguza 2 Wakorintho 1:21-22
5
2 Wakorintho 1:6
Ikiwa tunataabika, ni kwa ajili ya faraja na wokovu wenu; tukifarijiwa, ni kwa ajili ya faraja yenu, iwaleteayo saburi ya mateso yale yale yanayotupata.
Chunguza 2 Wakorintho 1:6
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video