Katika dhiki yake akamsihi Mwenyezi Mungu, Mungu wake, na kujinyenyekeza sana mbele za Mungu wa baba zake. Naye alipomwomba, Mwenyezi Mungu akaguswa na kule kusihi kwake na akasikiliza dua lake. Kwa hiyo akamrudisha Yerusalemu na kwenye ufalme wake. Ndipo Manase akatambua kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mungu.