Watu wa Ashdodi walipoamka asubuhi na mapema kesho yake, kumbe, wakamkuta Dagoni ameanguka kifudifudi mbele ya Sanduku la Mwenyezi Mungu! Wakamwinua Dagoni na kumrudisha mahali pake. Lakini asubuhi iliyofuata, walipoamka kumbe, walimkuta Dagoni ameanguka kifudifudi mbele ya Sanduku la Mwenyezi Mungu! Kichwa chake na mikono vilikuwa vimevunjwa, navyo vimelala kizingitini; ni kiwiliwili chake tu kilichokuwa kimebaki.