1
1 Samweli 17:45
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Daudi akamwambia yule Mfilisti. “Wewe unanijia na upanga, mkuki na fumo, lakini mimi ninakujia kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa majeshi ya Israeli, ambaye wewe umemtukana.
Linganisha
Chunguza 1 Samweli 17:45
2
1 Samweli 17:47
Wale wote waliokusanyika hapa watajua kuwa Mwenyezi Mungu haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; kwa kuwa vita ni vya Mwenyezi Mungu, naye atawatia ninyi wote mikononi mwetu.”
Chunguza 1 Samweli 17:47
3
1 Samweli 17:37
Mwenyezi Mungu ambaye aliniokoa toka katika makucha ya simba na makucha ya dubu ataniokoa kutoka mikono ya huyu Mfilisti.” Sauli akamwambia Daudi, “Nenda, naye Mwenyezi Mungu na awe pamoja nawe.”
Chunguza 1 Samweli 17:37
4
1 Samweli 17:46
Siku hii Mwenyezi Mungu atakutia mkononi mwangu, nami nitakupiga na kukukata kichwa chako. Leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya jeshi la Wafilisti, nayo dunia yote itajua kuwa yuko Mungu katika Israeli.
Chunguza 1 Samweli 17:46
5
1 Samweli 17:40
Kisha akachukua fimbo yake mkononi, akachagua mawe laini matano katika kijito, akayaweka kwenye kifuko ndani ya mfuko wake wa kichungaji, akiwa na kombeo yake mkononi mwake, akamkaribia yule Mfilisti.
Chunguza 1 Samweli 17:40
6
1 Samweli 17:32
Daudi akamwambia Sauli, “Mtu yeyote asife moyo kwa habari ya huyu Mfilisti; mtumishi wako ataenda kupigana naye.”
Chunguza 1 Samweli 17:32
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video