1
1 Nyakati 16:11
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Mtafuteni Mwenyezi Mungu na nguvu zake; utafuteni uso wake siku zote.
Linganisha
Chunguza 1 Nyakati 16:11
2
1 Nyakati 16:34
Mshukuruni Mwenyezi Mungu kwa kuwa ni mwema; fadhili zake zadumu milele.
Chunguza 1 Nyakati 16:34
3
1 Nyakati 16:8
Mshukuruni Mwenyezi Mungu, liitieni jina lake; wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda.
Chunguza 1 Nyakati 16:8
4
1 Nyakati 16:10
Lishangilieni jina lake takatifu; mioyo ya wale wanaomtafuta Mwenyezi Mungu na ifurahi.
Chunguza 1 Nyakati 16:10
5
1 Nyakati 16:12
Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya, miujiza yake na hukumu alizozitamka
Chunguza 1 Nyakati 16:12
6
1 Nyakati 16:9
Mwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa; waambieni matendo yake yote ya ajabu.
Chunguza 1 Nyakati 16:9
7
1 Nyakati 16:25
Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni mkuu, mwenye kustahili kusifiwa kuliko wote; yeye ni wa kuogopwa kuliko miungu yote.
Chunguza 1 Nyakati 16:25
8
1 Nyakati 16:29
mpeni Mwenyezi Mungu utukufu unaostahili jina lake. Leteni sadaka na mje katika nyua zake. Mwabuduni Mwenyezi Mungu katika uzuri wa utakatifu wake.
Chunguza 1 Nyakati 16:29
9
1 Nyakati 16:27
Fahari na enzi viko mbele yake; nguvu na utukufu vimo patakatifu pake.
Chunguza 1 Nyakati 16:27
10
1 Nyakati 16:23
Mwimbieni Mwenyezi Mungu dunia yote; tangazeni wokovu wake siku baada ya siku.
Chunguza 1 Nyakati 16:23
11
1 Nyakati 16:24
Tangazeni utukufu wake katika mataifa, matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote.
Chunguza 1 Nyakati 16:24
12
1 Nyakati 16:22
“Msiwaguse niliowapaka mafuta; msiwadhuru manabii wangu.”
Chunguza 1 Nyakati 16:22
13
1 Nyakati 16:26
Kwa maana miungu yote ya mataifa ni sanamu, lakini Mwenyezi Mungu aliziumba mbingu.
Chunguza 1 Nyakati 16:26
14
1 Nyakati 16:15
Hulikumbuka agano lake milele, neno ambalo aliamuru, kwa vizazi elfu
Chunguza 1 Nyakati 16:15
15
1 Nyakati 16:31
Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi; semeni katika mataifa, “Mwenyezi Mungu anatawala!”
Chunguza 1 Nyakati 16:31
16
1 Nyakati 16:36
Atukuzwe Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, tangu milele na hata milele. Nao watu wote wakasema, “Amen,” na “Msifuni Mwenyezi Mungu.”
Chunguza 1 Nyakati 16:36
17
1 Nyakati 16:28
Mpeni Mwenyezi Mungu, enyi jamaa za mataifa, mpeni Mwenyezi Mungu utukufu na nguvu
Chunguza 1 Nyakati 16:28
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video