Sauli alikufa kwa sababu hakuwa mwaminifu kwa Mwenyezi Mungu. Hakulishika neno la Mwenyezi Mungu, hata akataka shauri kwa mwaguzi kwa ajili ya uongozi, hakumuuliza Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo Mwenyezi Mungu alimuua, na ufalme akampa Daudi mwana wa Yese.