Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Ebr 10:24

Kupata Uhuru kutokana na Kufadhaika
Siku 5
Kufadhaika huwa, lakini hakufai kuyaendesha maisha yako. Kumpitia Kristo, tunaweza kuibadilisha, kuiona upya na kuitafsiri upya. Kama unapata changamoto na kufadhaika, angalia mpango huu wa Bibilia wa siku 5 ili ujifunze kupata uhuru na amani.

Hatua Zako za Mwanzo
Siku 5
Umefanya uamuzi wa kumfuata Yesu, sasa nini kinafuata? Mpango huu si orodha kamili ya kila kitu kinachokuja kutokana na uamuzi huo, lakini utakusaidia kuchukua hatua zako za kwanza.

Tabia
SIku 6
Mabadiliko si rahisi, lakini si kwamba hayawezekani. Kuanza tabia chache rahisi itabadilisha jinsi unajiona leo na kukugeuza uwe mtu ambaye ungependa kuwa kesho. Mpango huu wa Biblia wa Life.Church unatazama Maandiko ili kutengeneza tabia za kila siku ambazo zitadumu.

Ishi Maisha -Yaliyojaa Kusudi!
Siku 7
Maisha yenye kusudi na yaliyojaa furaha, hujengwa kwenye mahusiano, upendo na imani. Kama unataka njia iliyonyooka zaidi ya mpango wa Mungu kwa maisha yako, tumia mpango huu kukusaidia kuweka mkazo katika hilo lengo lako. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo Kwa Ukuaji na Kusudi” na David J. Swandt

Soma Biblia Kila Siku 10/2024
31 Siku
Soma Biblia Kila Siku 10/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania, Kutoka na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu