Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na 1 The 5:18

Mambo 7 ambayo Biblia inasema kuhusu Uzazi
Siku 7
Kulea watoto ni kazi kubwa, hata katika mazingira bora. Katika mpango huu wa ibada wa siku saba, wazazi wa ulimwengu halisi -ambao pia wametokea kuwa wafanyakazi wa YouVersion - wanatushirikisha jinsi wanavyotumia kanuni za neno la Mungu katika eneo hili muhimu katika maisha yao. Kila siku ya ibada hii inajumuisha taswira ya mstari unaoweza kuutumia kukusaidia kushirikia safari yako mwenyewe.

Mazungumzo na Mungu
Siku 12
Kuongea na Mungu ni furaha ya kuzama katika maisha ya maombi, ukisisitiza njia sahihi za kusikia sauti ya Mungu. Mungu anatutaka tufurahie mazungumzo endelevu pamoja naye katika maisha yetu yote - mazungumzo yanayoleta tofauti katika mwelekeo, mahusiano, na kusudi. Mpango huu umejaa uwazi, hadithi binafsi kuhusu kuufikia moyo wa Mungu. Anatupenda!

Maombi
Siku 21
Kujifunza namns ya kuomba vizuri, kutoka kwa maombi ya mwaminifi pia na maneno ya Yesu Mwenyewe. Kupata faraja ya kuendelea kuomba Mungu kila siku, pamoja na kudumu na uvumilivu. Chunguza mifano tupu, maombi ya uhaki wa mwenyewe, ikipimwa na maombi ya kweli ya walio na moyo safi. Omba bila kuacha.

Jolt ya Furaha
Siku 31
Biblia inatuambia kwamba "Katika uwepo wake kuna furaha tele" na kuwa "furaha ya Bwana ni nguvu yetu". Furaha sio hisia tu bali ni tunda la Roho na mojawapo ya silaha bora katika gala letu la kupigana na kuvunjika moyo, huzuni na kushindwa. Tumia siku 31 ukijifunza ni nini Biblia inasema kuhusu Furaha na kujiimarisha kuwa Mkristo mwenye Furaha bila wasi wasi.

Soma Biblia Kila Siku 5
Siku 31
Soma Biblia Kila Siku 5 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.

Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023
Siku 31
Soma Biblia Kila Siku/Machi 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wathesalonike na Yohana. Karibu kujiunga na mpango huu bure