Logotip YouVersion
Search Icon

Mattayo MT. 9

9
1AKAPANDA chomboni, akavuka, akafika mjini kwake. 2Wakamletea mgonjwa wa kupooza, amelala kitandani: na Yesu, akiona imani yao, akamwambia yule mgonjwa wa kupooza, Jipe moyo mkuu, mwanaugu; umeondolewa dhambi zako. 3Baadhi ya waandishi wakasema nafsini mwao, Huyu anakufuru. 4Nae Yesu, akijua mawazo yao, akasema, Jinsi gani mnawaza maovu mioyoni mwenu? 5Kwa maana vipi vyepesi, kusema, Umeondolewa dhambi zako; au kusema, Ondoka, ukaende? 6Lakini illi mjue ya kuwa Mwana wa Adamu yuna mamlaka katika dunia kuondoa dhambi, (amwambia yule mgonjwa wa kupooza) Ondoka, ujitwike kitanda chako, ukaende nyumbani kwako. 7Akaondoka, akaenda zuke nyumbani kwake. 8Makutano wakimwona, wakastaajabu, wakamtukuza Mungu, aliyewapa watu mamlaka ya jinsi hii.
9Yesu alipokuwa anaondoka kutoka huko akaona mtu amekeli fordhani, aitwae Mattayo, akamwambia, Nifuate. Akaondoka, akamfuata.
10Ikawa alipoketi ale ndani ya nyumba, wutoza ushuru wengi na wenye dhambi wakaja wakaketi pamoja na Yesu ua wanafunzi wake. 11Mafarisayo walipoona, wakawaambia wanafunzi wake, Kwa nini mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi? 12Nae Yesu akisikia, akawaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi. 13Lakini shikeni njia, mkajifunze maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka: kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi wapate kutubu.
14Wakati ule wanafunzi wa Yohana wakamwendea, wakinena, Kwa nini sisi na Mafarisayo twafunga marra nyingi, bali wanafunzi wako hawafungi? 15Yesu akawaambia, Wana wa arusi wawezaje kuomboleza, maadam Bwana arusi yupo pamoja nao? Lakini siku zitakuja atakapoondolewa bwana arusi; udipo watakapofunga. 16Hakuna mtu atiae kipande cha nguo mpya katika vazi kuukuu; maana kile kilichotiwa huondoa kipande cha lile vazi, likazidi kutatuka. 17Wala watu hawatii divai mpya katika viriba vikuukuu; ikiwa watia, vile viriba hupasuka, divai ikamwagika, vile viriba vikaharibika: bali hutia divai mpya katika viriba vipya, vikahifadhika vyote.
18Alipokuwa akiwaambia haya, yuaja jumbe mmoja, akamsujudia, akinena, Binti yangu udio kwanza afe: lakini njoo, uweke mkono wako juu yake, uae atapona. 19Akaondoka Yesu, akamfuata, pamoja na wanafunzi wake. 20Na mwanamke, aliyekuwa na ugonjwa wa kutoka damu muda wa miaka thenashara, alikuja kwa nyuma, akagusa upindo wa vazi lake: 21kwa maana alisema kimoyomoyo, Nikigusa tu upindo wa vazi lake nitapona. 22Yesu akageuka, akamwona, akamwambia, Jipe moyo mkuu, binti yangu; imani yako imekuponya. Yule mwanamke akapona tangu saa ile. 23Yesu alipofika nyumbani kwa yule jumbe, akaona wapiga filimbi, na makutano wakifanya maombolezo, 24akawaambia, Ondokeni: kwa maana kijana hakufa, amelala tu. Wakamcheka sana. 25Hatta makutano walipoondoshwa, akaingia, akamshika mkono wake; yule kijana akasimama. 26Zikaenea khabari hizi katika inchi ile yote.
27Yesu alipokuwa anaondoka kutoka huko, vipofu wawili wakamfuata wakipaaza sauti, wakinena. Uturehemu, Ee mwana wa Daud. 28Alipolika nyumbani, wale vipofu wakamwendea: Yesu akawaambia. Mnaamini kwamba naweza kufanya haya? Wakamwambia, Naam, Bwana. 29Marra akawagusa macho yao, akanena, Kwa kadiri ya imani yenu mpate. 30Macho yao yakafumbuka. Yesu akawaagiza kwa nguvu, akinena, Angalieni hatta mtu mmoja asijue.
31Lakini wakatoka, wakaeneza khabari zake katika inchi ile yote.
32Hatta wale walipokuwa wakitoka, wakamletea mtu bubu mwenye pepo. 33Na pepo alipofukuzwa, yule bubu akasema, makutano wakastaajabu, wakanena, Haijaonekana hivi katika Israeli wakati wo wote. 34Lakini Mafarisayo wakanena, Kwa mkuu wa pepo afukuza pepo.
35Na Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masunagogi yao, akikhubiri injili ya ufalme, akiponya magonjwa yote na dhaifu zote katika watu. 36Na alipowaona makutano, akawahurumia, kwa maana walikuwa wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchunga. 37Ndipo akawaambia wanafunzi wake, Mavuno ni makubwa, bali watenda kazi wachache. 38Bassi mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake.

Currently Selected:

Mattayo MT. 9: SWZZB1921

Označeno

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in