Mattayo MT. 5
5
1NAE akivaona makutano, akapanda mlimani; na alipokwisha kuketi, wanafunzi wake wakamjia; 2akafunua kinywa chake, akawafundisha, akinena,
3Wa kheri walio maskini wa roho; maana ufalme wa mbinguni ni wao.
4Wa kheri wenye huzuni: maana hawo watafarajika.
5Wa kheri wenye upole: maana hawo watairithi inchi.
6Wa kheri wenye njaa na kiu ya haki: maana hawo watashiba.
7Wa kheri wenye rehema: maana hawo watarehemiwa.
8Wa kheri walio na moyo safi; maana hawo watamwona Mungu.
9Wa kheri wasuluhishi: maana hawo watakwitwa wana wa Mungu.
10Wa kheri wateswao kwa ajili ya haki: maana ufalme wa mbinguni ni wao.
11M kheri ninyi watakapowatukana na kuwatesa na kuwanenea killa neno baya kwa uwongo, kwa ajili yangu. 12Furahini, shangilieni: kwakuwa thawabu yenu nyingi mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowatesa manabii waliokuwa kabla yenu.
13Ninyi ni chumvi ya dunia: lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwani ikolee? Haifai tena kabisa, illa kufupwa nje na kukanyagwa na watu. 14Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kustirika ukiwa juu ya mlima. 15Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya kibaba, bali juu ya kibao cha kuwekea taa; nayo yaangaza wote waliomo nyumbani. 16Vivi hivi nuru yenu iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wakamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.
17Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. 18Kwa maana, amin nawaambieni, Mpaka mbingu na inchi zitakapoondoka, yodi moja na nukta moja ya torati haitaondoka, mpaka yote yatimie.
19Bassi mtu atakaevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha wafu hivi, atakwitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni: bali mtu atakaezitenda na kufundisha, huyu afakwitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni. 20Maana nawaambieni, Haki yenu isipozidi kuliko haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
21Mmesikia watu wa kale walivyoanibiwa, Usiue; na mtu akiua, itampasa hukumu. 22Bali mimi nawaambiem, Killa amwoneae ndugu yake ghadhabu bila sababu, itampasa hukumu; na mtu akimwambia ndugu yake, Haka, itampasa baraza; na mtu akinena, Mpumbavu, itampasa jebannum ya moto. 23Bassi ukileta sadaka yako madhbahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako, 24iache sadaka yako mbele ya madbbahu, nenda zako, kwanza patana na ndugu yako, kisha rudi utoe sadaka yako, 25Patana na mshtaki wako upesi, wakati uwapo pamoja nae njiani; yule mshtaki asije akakupeleka kwa kadhi, kadhi akakutia mkononi mwa askari, ukatupwa kifungoni. 26Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hatta uishe kulipa pesa ya mwisho.
27Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usizini: 28Bali mimi miwaambieni, Killa mtu atazamae mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini nae moyoni mwake. 29Jicho lako la kuume likikukosesha, lingʼoe ulitupe mbali nawe: kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehannum. 30Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe: kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee, wala mwili wako mzima usitupwe katika jehannum.
31Waliambiwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe khati ya talaka; 32bali mimi nawaambieni, Killa mtu amwachae mkewe, isipokuwa kwa khabari ya asharati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.
33Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usifanye zuli, bali mtimizie Bwana nyapo zako; 34bali mimi nawaambieni, Usiape kabisa; hatta kwa mbingu, kwa maana ndio kiti cha enzi cha Mungu; 35wala kwa inchi, kwa maana ndio pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemi, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu. 36Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unyele mmoja kuwa mwenpe au mwensi. 37Bali maneno yenu yawe, Ndio, ndio; Sio, sio: kwa kuwa izidiyo haya yatoka kwa yule mwovu.
38Mmesikia walivyoambiwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino: 39bali mimi nawaambieni, Msishindane na mtu mwovu; bali mtu akupigae shavu la kuume, mgeuzie na la pili. 40Na mtu atakae kukushtaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho. 41Na mtu atakaekutumikisha maili moja, nenda nae mbili. 42Akuombae, mpe; nae atakae kukopa kwako, usimpe kisogo.
43Mmesikia walivyoambiwa, Mpende jirani yako, na, Mchukie adui yako: 44bali mimi nawaambieni, Wapendeni adui zenu, wabarikini wanaowalaani, watendeni mema wanaowachukia, waombeeni wanaowatendea ukorofi, na kuwatesa; 45illi mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni: maana yeye jua lake huwazushia waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. 46Maana mkiwapenda wanaowapendani, mwapata thawabu gani? Hatta watoza ushuru, je, nao hawafanyi yayo hayo? 47Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziyada? Hatta wattoza ushuru, je, nao hawafanyi kama hayo? 48Bassi mwe ninyi wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
Currently Selected:
Mattayo MT. 5: SWZZB1921
Označeno
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.