YouVersion Logo
Search Icon

Usionee Haya InjiliSample

Usionee Haya Injili

DAY 2 OF 4

Linda Injili

Wakati ukweli wa injili unapungua katika miji na vijiji vyetu, maandiko yanatuita tuilinde injili. Biblia inasema, "Ilinde ile amana nzuri kwa Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu."

Njia bora ya kuilinda ni kwa kuipitisha kwa kizazi kijacho. Hatuko wageni kwa mambo kupitishwa kwetu. Kwa hakika, tamaduni zetu za Kiafrika zimepitishwa kutoka kizazi hadi kizazi. Injili pia imepitishwa kwetu tangu siku za Bwana wetu, Yesu Kristo. Kuipitisha injili isiyopotoshwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kumehakikisha kwamba tunaweza kuisikia leo. Ili kizazi kijacho kiweze kusikia injili, tunaitwa pia kuwakambithi watu waaminifu ambao wataweza kufundisha wengine pia Kwa njia hii, tutaweza kuilinda injili.

Day 1Day 3

About this Plan

Usionee Haya Injili

Tunaishi katika nyakati ambapo Injili ya kweli inaonekana kupoteza mvuto wake. Wengi hukimbilia kusikia yale yanayowapendeza, huku wachungaji wakijaribu kuifanya Injili ivutie zaidi. Kwa sababu hiyo, wengi wanaionea aibu Injili. Katika siku tano zijazo, tutatembea na Paulo kupitia 2 Timotheo, ambako anatuhimiza tusiionee aibu Injili, bali tuwe tayari kuteseka kwa ajili yake, kuilinda, kuendelea nayo, na kuihubiri.

More