YouVersion Logo
Search Icon

Tafakari Kuhusu HakiSample

Tafakari Kuhusu Haki

DAY 6 OF 31

‘Dini inanuka, lakini injili ni mlipuko.’ Hii ilikuwa kauli mbiu ya kampeni ya uinjilisti wakati wa kiangazi mwaka 2000. Wakristo ndiyo walio shituka zaidi.

Je, sisi bado ni mifano mizuri? Je, dini yetu huwafanya watu waone wivu? Miaka elfu mbili iliyopita, Yakobo aliandika kuhusu umuhimu wa kuuzuia ulimi wa mtu. Kwa bahati mbaya hakuna mmoja wetu anayeepushwa na ukweli huu ‘unaonuka’, migogoro na migongano ili kutunza nafasi ya mtu au uwezo wa mtu.

Lakini kama tukijiruhusu kuguswa na upendo wa Mungu, tunaweza kuacha nje vitendo vilivyopendekezwa katika tafsiri ya Yakobo 1:27: kumwokoa, kusaidia, kutunza, kutembelea, kufikia. Hii ndiyo maana injili hii ni mlipuko!

Nafahamu matendo haya vizuri. Kama mama yameingizwa ndani yangu, nami nayatumia kwa furaha na bila kizuizi! Kuokoa, kusaidia, kutunza. kutembelea, kuwafikia.

Changamoto: Washirikishe wengine injili kama chakula ambacho mtu anakihitaji sana. Hata kama kwa mtazamo wa kwanza inaonekana kuwa ya kuchukiza au haina uhakika, upendo wa Mungu ni mlipuko kama wakishirikishwa wengine.

Maombi: Bwana, nisaidie kubeba na kuwashirikisha wengine thamani ya upendo zaidi ya wajibu au matarajio.

Scripture

Day 5Day 7

About this Plan

Tafakari Kuhusu Haki

Mfululizo wa tafakari ya kila siku kuhusu haki, ulioandikwa na wanawake kutoka kote katika dunia ya Jeshi la Wokovu. Maswala ya haki ya jamii yako mbele sana ya mawazo yetu siku hizi. Mkusanyo huu wa tafakari kuhusu haki ya jamii umeandikwa na wanawake kutoka kote duniani wenye nia na hamu ya kuwasaidia wengine katika jina la Kristo.

More