Tafakari Kuhusu HakiSample

Nimekuwa nakaa na maneno ya Mithali 3:27-28 kwa muda wakati wa Sabato, na vile vile wakati wa kusoma kuhusu umuhimu wa kuheshimu kila mara, Sabato ya Mungu iliyoteuliwa.
Vifungu hivi vinaweza kuchemsha ndani yangu ‘mwito wa wajibu’ ninapokuwa tayari nimechoka ‘kutenda mema’. Kwa mfano, napenda kupika chakula na kukipeleka kwa mtu ambaye amefiwa mda si mrefu, lakini hili limetokea mara chache katika shughuli za huduma ya kanisa. Vifungu hivi vinaweza kuniacha mimi na hisia ya hatia au kujisikia sifanyi kwa kutosheleza.
Hata hivyo, ‘kutenda kwa haki’ vile vile ni pamoja na kutenda vema kwa makusudi kwetu wenyewe. Kitu hutendeka kwetu tunapoheshimu pumziko la Sabato. Walter Brueggemann anaeleza: ‘Sabato sio tu pumziko linaloburudisha. Ni pumziko linalobadilisha.’ Tunaporudi kwenye kazi yetu ya kila siku tunakuwa tuko vizuri zaidi, tumepumzika na tuwasikivu. Tunaweza sana kusema, ‘Napatikana!’
Changamoto: Najiuliza kama unajisikia kuvutwa kuchunguza kwa kina mwaliko wa Mungu wa kuheshimu pumziko la Sabato? Hili linaweza kukubadilisha namna gani na kukufanya uwe unapatikana zaidi kutenda mara moja?
Maombi: Bwana, kwa sababu ya wengine na mimi mwenyewe, nisaidie nikubali na nipende zawadi yako ya Sabato. Hebu kwa wakati ‘matendo’ yangu yatokane na hekalu hili.
Scripture
About this Plan

Mfululizo wa tafakari ya kila siku kuhusu haki, ulioandikwa na wanawake kutoka kote katika dunia ya Jeshi la Wokovu. Maswala ya haki ya jamii yako mbele sana ya mawazo yetu siku hizi. Mkusanyo huu wa tafakari kuhusu haki ya jamii umeandikwa na wanawake kutoka kote duniani wenye nia na hamu ya kuwasaidia wengine katika jina la Kristo.
More
Related Plans

The Joy

Go Into All the World

God's Great Story

Heart-Tongues

Acts 20 | Encouragement in Goodbyes

Seeing Disabilities Through God's Eyes: A 5-Day Devotional With Sandra Peoples

Winter Warm-Up

Spiritual Training: The Discipline of Fasting and Solitude

Over the Fence: Lessons From Ephesus
