Njia Ya Mungu Ya MafanikioSample
Katika ulimwengu wa kiroho, mafanikio yanapatikana katika kutimiza kusudi la Mungu katika maisha yako. Hiyo ndiyo tafsiri ya kibiblia ya mafanikio. Katika tamaduni zetu leo, kuna maelezo kadhaa yenye makosa ya maana ya kufanikiwa. Baadhi ya watu hudhani kuwa mafanikio yanatokana na kiasi cha pesa ulichonacho. Wengine huiwekea msingi kwa cheo ulichopanda kazini. Siku hizi za leo, inaweza kufafanuliwa na idadi ya wafuasi ulio nao kwenye mitandao ya kijamii. Lakini tatizo la mawazo haya yote ni kwamba hayatokani na kiwango cha Mungu cha mafanikio.
Yesu alitupa ufafanuzi wa mafanikio aliposema, “Nimekutukuza duniani, nikiisha kuimaliza kazi uliyonipa niifanye” (Yohana 17:4).
Paulo alisema jambo lile lile kwa njia tofauti alipoandika maneno haya: “Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, imani nimeilinda” (2 Timotheo 4:7).
Kwa hakika, Mungu alimwambia Yoshua kwamba mafanikio yake yalitegemea kabisa kutafakari kwake kwa makini Neno la Mungu pamoja na kupanga maamuzi yake na matendo yake chini yake (Yoshua 1:8). Mafanikio yanahusisha kutimiza kile ambacho Mungu amekuitia utende.
Je, tafsiri yako binafsi ya mafanikio ni nini?
Je, tafsiri yako inalinganishwaje na ufafanuzi wa Mungu?
Scripture
About this Plan
Kila mtu anatafuta mafanikio, lakini wengi hawayapati kwa sababu wanachofuata ni ufahamu potofu wa nini maana ya kuishi maisha ya mafanikio. Ili kupata mafanikio ya kweli unahitaji kuweka macho yako katika ufafanuzi wa Mungu wa maana yake. Mruhusu mwandishi wa vitabu vinavyouzwa sana Tony Evans akuonyeshe njia ya mafanikio ya kweli ya ufalme na jinsi unavyoweza kuipata.
More