YouVersion Logo
Search Icon

Plan Info

Upendo Wa BureSample

Upendo Wa Bure

DAY 2 OF 5

Kutoka Upendo wa Bure hadi Maisha Hovyo Kijana aliyekuwa anelekea kuwa Mwana Mpotevu, ambaye alikuwa mdogo wa ndugu wawili, alitenda jambo la kuhuzunisha sana, jambo la kumkosea heshima Baba yake na kudharau mapenzi ya dhati au ya bure Baba yake alimpa mwanawe. Kwa ufupi, alimwambia Baba yake”Ninajua bado ungali hai, lakini, siwezi kungoja tena - ninataka urithi wangu sasa.” Baba yake hakuwa na jukumu la kugawa mali yake lakini, kwa kitendo cha kushangaza, alikubali ombi la mwanawe na kugawa mali yake vilivyo, kisha akampa mwanawe mdogo urithi wake. Kwa muda usiokuwa mrefu, Kijana huyu alichukuwa hela zake zote na kujishughulisha na maisha ya hali ya juu. Aliishi maisha ya anasa, katika Jiji kuu. Ingawa Bibilia haifafanui kikamilifu shughuli zake huko mjini, tunapata kujua kwamba “akakusanya vitu vyote alivyokuwa navyo akaenda nchi ya mbali akaitapanya mali yake kwa maisha ya anasa.” (Luka 15:13) Inamaanisha kwamba alikuwa anaishi maisha hovyo - bila fikra za kesho, bila kujali kamwe ila kufuata msisimko alioupata katika nyakati fupi au chache za raha. Hakuwajli familia/jamii yake. Hakujalishwa na afya yake, kazi yake, sifa zake au mfano aliotoa kwa jumuiya yake - yote yalikuwa duni. Aliishi kupata msisimko wa raha za kimwili. Mtazamo huu wa maisha unaoenezwa katika matelevisheni na filamu ni jinsi watu wengi wanvyoishi maisha yao - lakini, mtindo huu ni wa ubinafsi mkuu na kutojibika. Tabia hii hailengi mbali kwenye fikira za mtu, ni tabia za mtu ambaye hajakomaa na ni tabia haribifu sana inayoelekeza mtu katika njia alioypitia Mwana Mpotevu na kukosa kabisa lengo la maisha. Maisha haya ya hovyo yanatilia maanani raha na starehe na msisimko wa wakati mfupi tu, kuliko mambo yote mengine yenye msingi bora. Niamini kwa kweli, ingawa Mwana Mpotevu alikuwa anapiga debe la maisha ya uharibifu, alipata kujuta.

Scripture

Day 1Day 3

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy