BibleProject | Kumwamini Mungu katika MatesoPrøve

BibleProject | Kumwamini Mungu katika Mateso

Dag 2 av 6

Kitabu cha Ayubu kinapoanza, tunapelekwa mbinguni ambapo Mungu anaendesha kikao na malaika (taswira ya kawaida katika Agano la Kale inayoonyesha jinsi Mungu huendesha ulimwengu). Miongoni mwa malaika, pamesimama kiumbe aitwaye "shetani", ambayo kwa Kiebrania inamaanisha "mshtaki" au "anayeshtaki". Na katika kikao, Mungu anasema kuwa Ayubu ni mwandamu mwenye haki. Lakini shetani hakubaliani na hii hoja. Anashuku nia ya Ayubu, akisema kwamba Ayubu hutii tu ili kupata baraka na ulinzi wa Mungu. Anaamini kuwa Mungu akiruhusu Ayubu kuteseka, Ayubu atamlaani Mungu. Hivyo shetani anapendekeza majaribu kuona ikiwa Ayubu atafanya hivyo, na cha kushangaza Mungu anakubali. Japo anampa masharti, anamruhusu asababishe mateso kwa Ayubu.

Huenda wengi wetu tunajiuliza maswali. Hii ni sawa kweli? Je, namna ya Mungu ya kuendesha ulimwengu kweli ni ya busara na haki? Hatuko peke yetu katika kuchanganyikiwa huku. Ayubu pia anauliza maswali haya. Hivyo hebu tuendelee kusoma. Tenga muda utafakari yafuatayo unaposoma Maandiko leo.

Tafakari:
1) Je, mateso yanaweza kuonyesha vipi nia yetu ya kumtumikia Mungu?
2) Mtu angekushtaki kuwa una nia mbaya, je, ungependa fursa ya kuthibitisha kuwa anachosema sio kweli?
3) Je, Yesu aliteseka vipi aliposhtakiwa kwa uongo? Je, alishinda vipi?

Skriften

Dag 1Dag 3

Om denne planen

BibleProject | Kumwamini Mungu katika Mateso

Je, tunawezaje kumwamini Mungu hata pale tunapoteseka bila kustahili? Jiunge nasi katika muongozo huu wa wa siku zita unaotazama simulizi ya Ayubu na ufahamu jinsi kuamini hekima ya Mungu kunaonekaje hata katika vipindi tunapokumbana na magumu.

More