YouVersion logotips
Meklēt ikonu

Mattayo MT. 7

7
1MSIHUKUMU, illi msihukumiwe 2Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa: na kipimo kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa. 3Nawe, ya nini kukitazama kibanzi kilicho katika jicho la ndugu yako, na boriti iliyo katika jicho lako huiangalii? 4Au utamwambiaje ndugu yako, Niache niondoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! imo boriti ndani ya jicho lako? 5Mnaflki, iondoe kwanza ile boriti katika jicho lako; ndipo utakapoona sana hatta kukiondoa kibanzi katika jicho la ndugu yako.
6Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararueni.
7Ombeni na mtapewa; tafuteni na mtaona; bisheni na mtafunguliwa: 8kwa maaua killa aombae hupokea; nae atafutae huona, nae abishae alafunguliwa. 9Au mtu yupi katika ninyi, ambae, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe? 10Au akiomba samaki, atampa nyoka? 11Kama ninyi, bassi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! si zaidi Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wamwombao? 12Bassi yo yote mtakayo kutendewa na watu, nanyi mwatendee vivyo hivyo: maana hiyo ndiyo torati na manabii.
13Ingieni kwa kupita mlango ulio mwembamba: maana ujia iendayo hatta upotevu ni pana, na mlango wake mpana, na wengi waingiao kwa mlango huo. 14Bali njia ni nyembamba iendayo hatta uzima, na mlango wake ni mwembamba: nao waionao ni wachache.
15Jihadharini na manabii wa uwongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa wa mwitu wakali. 16Mtawalambua kwa matunda yao. Je, watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? 17Vivyo hivyo killa mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti uliopea huzaa matunda hafifu. 18Mti mwema hauwezi kuzaa matunda hafifu, wala mti uliopea kuzaa matunda mazuri. 19Killa mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. 20Bassi kwa matunda yao mtawatambua. 21Siye killa mtu aniambiae, Bwana, Bwana, atakaeingia katika ufalme wa mbinguni; hali yeye afanyae mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 22Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kufukuza pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? 23Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwafahamu ninyi wakati wo wote: ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu. 24Bassi killa asikiae haya maneno yangu, na kuyafanya, nitamfananisha na mtu mwenye akili aliyejenga nyumba vake juu ya mwamba: 25mvua ikanya, maji mengi yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa katika mwamba.
26Na killa asikiae haya maneno yangu, asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, alivejenga nyumba yake katika mchanga; 27mvua ikanya, maji mengi yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; anguko lake likawa kubwa.
28Ikawa, Yesu alipomaliza maneno haya, makutano wakashangaa kwa mafundisho yake: 29kwa maana alikuwa akiwafundisha kwa namna ya mwenye mamlaka, wala si kama waandishi wao.

Pašlaik izvēlēts:

Mattayo MT. 7: SWZZB1921

Izceltais

Dalīties

Kopēt

None

Vai vēlies, lai tevis izceltie teksti tiktu saglabāti visās tavās ierīcēs? Reģistrējieties vai pierakstieties

Lai personalizētu tavu pieredzi, YouVersion izmanto sīkfailus. Izmantojot mūsu vietni, tu piekrīti, ka mēs izmantojam sīkfailus, kā aprakstīts mūsu Privātuma politikā