Mathayo 14:18-19
Mathayo 14:18-19 TKU
Yesu akasema, “Leteni kwangu mikate na samaki.” Kisha akawaambia watu waketi chini kwenye nyasi. Akaichukua mikate mitano na samaki wawili. Akatazama mbinguni na akamshukuru Mungu kwa ajili ya chakula. Kisha akaivunja mikate katika vipande, akawapa wafuasi wake nao wakawapa watu chakula.