Yohana 11:43-44
Yohana 11:43-44 TKU
Baada ya Yesu kusema hivi akaita kwa sauti kubwa, “Lazaro, toka nje!” Yule mtu aliyekuwa amekufa akatoka nje, mikono na miguu yake ilikuwa imefungwa sanda. Uso wake ulikuwa umefunikwa kwa kitambaa. Yesu akawaambia watu, “Mfungueni hizo sanda na kumwacha aende.”