Mwa 15

15
Agano la Mungu na Abramu
1 # Mwa 46:2; Isa 41:10; Zab 58:11; 84:11; Ebr 11:6 Baada ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana. 2Abramu akasema, Ee Bwana MUNGU, utanipa nini, nami naenda zangu hali sina mtoto, na atakayeimiliki nyumba yangu ni huyu Eliezeri, Mdameski? 3Abramu akasema, Tazama, hukunipa uzao, na mtu aliyezaliwa nyumbani mwangu ndiye mrithi wangu.
4 # Mwa 17:16; 2 Sam 7:12 Nalo neno la BWANA likamjia likinena, Huyu hatakurithi, bali atakayetoka katika viuno vyako ndiye atakayekurithi. 5#Rum 4:18; Ebr 11:12; Zab 147:4; Kut 32:13Akamleta nje, akasema, Tazama sasa mbinguni, kazihesabu nyota, kama ukiweza kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako. 6#Rum 4:3-6,20-25; Zab 106:31; Gal 3:6; Yak 2:23Akamwamini BWANA, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki. 7#Mdo 7:2Kisha akamwambia, Mimi ni BWANA, niliyekuleta kutoka Uru wa Wakaldayo nikupe nchi hii ili uirithi.
8 # Amu 6:36-40; 1 Sam 14:9,10; 2 Fal 20:8; Lk 1:18 Akasema, Ee Bwana MUNGU, nipateje kujua ya kwamba nitairithi? 9Akamwambia, Unipatie ndama wa miaka mitatu, na mbuzi mke wa miaka mitatu, na kondoo mume wa miaka mitatu, na hua, na mwana njiwa. 10Akampatia hao wote, akawapasua vipande viwili, akaweka kila kipande kuelekea mwenzake, ila ndege hakuwapasua. 11Hata tai walipotua juu ya mizoga Abramu akawafukuza. 12#Ayu 4:13,14; Mwa 2:21Na jua lilipokuwa likichwa usingizi mzito ulimshika Abramu, hofu ya giza kuu ikamwangukia. 13#Kut 1:1-14; 12:40; Mdo 7:6BWANA akamwambia Abramu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, watawatumikia watu wale, nao watateswa muda wa miaka mia nne. 14#Kut 6:6; 7:14; Kut 12:40-41; Mdo 7:7Hata na taifa lile, watakaowatumikia, nitawahukumu; baadaye watatoka na mali mengi. 15#Mwa 25:8; Ayu 5:26; Ebr 11:13Lakini wewe utakwenda kwa baba zako kwa amani, utazikwa katika uzee mwema. 16#Mt 23:32; 1 The 2:16; 2 Pet 3:8,9Na kizazi cha nne kitarudi hapa, maana haujatimia uovu wa Waamori bado. 17Ikawa, jua lilipokuchwa likawa giza, tazama, tanuru ya moshi na mwenge unaowaka ulipita kati ya vile vipande vya nyama.
18 # Mdo 7:5; Mwa 17:8; Kum 1:7; Hes 34:3; 2 Nya 9:26; Neh 9:8; Zab 105:11 Siku ile BWANA akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati, 19Mkeni, na Mkenizi, na Mkadmoni, 20na Mhiti, na Mperizi, na Mrefai, 21na Mwamori, na Mkanaani, na Mgirgashi, na Myebusi.

Currently Selected:

Mwa 15: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in