1
Mwanzo 32:28
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Ndipo yule mtu akasema, “Jina lako halitakuwa tena Yakobo, bali Israeli, kwa sababu umeshindana na Mungu na watu pia, nawe umeshinda.”
Lee anya n'etiti ihe abụọ
Nyochaa Mwanzo 32:28
2
Mwanzo 32:26
Ndipo yule mtu akasema, “Niache niende, kwa kuwa ni mapambazuko.” Lakini Yakobo akajibu, “Sitakuacha uende usiponibariki.”
Nyochaa Mwanzo 32:26
3
Mwanzo 32:24
Kwa hiyo Yakobo akaachwa peke yake; naye mtu mmoja akashikana naye mweleka hadi mapambazuko.
Nyochaa Mwanzo 32:24
4
Mwanzo 32:30
Kwa hiyo Yakobo akapaita mahali pale Penieli, akisema, “Ni kwa sababu nimemwona Mungu uso kwa uso, na bado uhai wangu umehifadhiwa.”
Nyochaa Mwanzo 32:30
5
Mwanzo 32:25
Yule mtu alipoona kuwa hawezi kumshinda, aligusa kiungio cha nyonga ya Yakobo; kwa hiyo nyonga yake ikateguka alipokuwa akishikana mweleka na yule mtu.
Nyochaa Mwanzo 32:25
6
Mwanzo 32:27
Yule mtu akamuuliza, “Jina lako ni nani?” Akamjibu, “Ni Yakobo.”
Nyochaa Mwanzo 32:27
7
Mwanzo 32:29
Yakobo akasema, “Tafadhali niambie jina lako.” Lakini akajibu, “Kwa nini kuniuliza Jina langu?” Ndipo akambariki huko.
Nyochaa Mwanzo 32:29
8
Mwanzo 32:10
Sistahili fadhili na uaminifu wako wote ulionitendea mimi, mtumishi wako. Nilikuwa na fimbo tu mkononi mwangu nilipovuka mto huu wa Yordani, lakini sasa nimekuwa makundi mawili.
Nyochaa Mwanzo 32:10
9
Mwanzo 32:32
Kwa hiyo hadi leo Waisraeli hawali mshipa ulioungana na kiungio cha nyonga, kwa sababu kiungio cha nyonga ya Yakobo kiliteguliwa karibu na mshipa huo.
Nyochaa Mwanzo 32:32
10
Mwanzo 32:9
Ndipo Yakobo akaomba, “Ee Mungu wa baba yangu Ibrahimu, Mungu wa baba yangu Isaka, Ee Mwenyezi Mungu, ndiwe uliniambia, ‘Rudi katika nchi yako na jamaa yako, nami nitakufanya ustawi.’
Nyochaa Mwanzo 32:9
11
Mwanzo 32:11
Nakuomba uniokoe kutoka kwa mkono wa ndugu yangu Esau, kwa maana ninaogopa kuwa atakuja kunishambulia, pia kina mama pamoja na watoto wao.
Nyochaa Mwanzo 32:11
Ulo
Akwụkwọ Nsọ
Atụmatụ
Vidiyo