1 Mose 8
8
Mwisho wa mafuriko ya maji.
1Kisha Mungu akamkumbuka Noa na wale nyama wote nao nyama wa nyumbani waliokuwa naye chomboni; ndipo, Mungu alipovumisha upepo juu ya nchi; kwa hiyo maji yakaanza kupwa.#1 Mose 7:11-12. 2Nazo chemchemi za vilindini zikazibwa, nayo madirisha ya mbinguni yakafungwa, nazo mvua zilizotoka mbinguni zikakomeshwa. 3Kwa hiyo maji yakaanza kutoka tena juu ya nchi, yakaenda vivyo hivyo na kurudi mahali pao, baada ya siku 150 yakawa yamepunguka. 4Kisha kile chombo kikaja kutua kileleni kwa milima ya Ararati katika mwezi wa saba siku ya kumi na saba ya mwezi. 5Nayo maji yakawa yakiendelea kupunguka mpaka mwezi wa kumi. Siku ya kwanza ya mwezi katika mwezi wa kumi ndipo, vichwa vya milima vilipotokea. 6Siku 40 zilipopita tena, Noa akafungua dirisha la chombo, alilolifanya, 7akatoa kunguru; huyu akaruka kwenda na kurudi kwenda na kurudi, mpaka maji yakikauka katika nchi. 8Kisha akatoa njiwa kwake, aone, kama maji yamekauka katika nchi. 9Huyo njiwa asipoona pa kutulia kwa nyayo za miguu yake akarudi kwake chomboni, kwani maji yalikuwa yangaliko juu ya nchi yote; naye akautoa mkono wake, akamchukua na kumwingiza kwake chomboni. 10Akangoja tena siku saba nyingine, kisha akatoa tena njiwa mle chomboni. 11Huyu njiwa aliporudi kwake saa za jioni, akaona mdomoni mwake jani la mchekele, alilolivunja. Ndipo, Noa alipotambua, ya kuwa maji yamepunguaka katika nchi. 12Akangoja tena siku saba nyingine, akatoa tena njiwa, naye hakurudi tena kwake. 13Ikawa katika mwaka wa 601 katika mwezi wa kwanza siku ya kwanza ya mwezi, ndipo, maji yalipokauka na kutoweka juu ya nchi. Naye Noa alipokiondoa kipaa cha chombo kutazama, akaona, ya kuwa nchi imekauka juu. 14Katika mwezi wa pili siku ya ishirini na saba ya mwezi nchi ilikuwa imekauka kabisa.
Shukrani ya Noa.
15Mungu akasema na Noa kwamba: 16Toka chomboni, wewe na mkeo na wanao na wake wa wanao walio pamoja na wewe! 17Nao nyama wote walioko kwako, wao wote wenye miili: ndege na nyama na wadudu wote waliotambaa katika nchi watoe pamoja na wewe, wajiendee po pote katika nchi, wapate kuzaa na kuwa wengi tena katika nchi!#1 Mose 1:22,28. 18Ndipo, Noa alipotoka na wanawe na mkewe na wake wa wanawe waliokuwa naye;#2 Petr. 2:5. 19tena nyama wote na wadudu wote na ndege wote nao wote waliotambaa katika nchi wakatoka chomboni, walimokuwa, kabila kwa kabila. 20Kisha Noa akamjengea Bwana pa kumtambikia, akatoa wengine katika nyama wote wa nyumbani wanaotakata na katika ndege wote wanaotakata, akawatolea hapo pa kumtambikia Bwana kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima.#1 Mose 7:2.
Kiagio cha Mungu.
21Bwana aliposikia huo mnuko wa kumpendeza Bwana akasema moyoni mwake: Sitaiapiza nchi tena kwa ajili ya watu, kwani mawazo ya mioyo ya watu ni mabaya tangu utoto wao, wala sitawapiga tena wote walio hai, kama nilivyofanya.#1 Mose 6:5; Sh. 14:3; Iy. 14:4; Mat. 15:19; Rom. 3:23; Yes. 54:9. 22Siku zote, nchi itakazokuwapo, hakutakoma tena kupanda na kuvuna, baridi na jua kali, kipupwe na kiangazi, mchana na usiku.#Yer. 33:20,25.
Jelenleg kiválasztva:
1 Mose 8: SRB37
Kiemelés
Megosztás
Másolás
Szeretnéd, hogy a kiemeléseid minden eszközödön megjelenjenek? Regisztrálj vagy jelentkezz be
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.