1 Mose 12
12
Aburamu anaitwa na Mungu.
1Bwana akamwambia Aburamu: Toka katika nchi yako kwenye ndugu zako namo nyumbani mwa baba yako, uende katika nchi, nitakayokuonyesha!#Tume. 7:3; Ebr. 11:8. 2Nitakufanya kuwa taifa kubwa, nitakubariki na kulikuza jina lako, uwe mbaraka.#1 Mose 24:1,35; Sh. 72:17. 3Nitawabariki watakaokubariki, naye atakayekuapiza nitamwapiza. Mwako ndimo, koo zote za nchini zitakamobarikiwa.#2 Mose 23:22; 1 Mose 18:18; 22:18; 26:4; 28:14; Tume. 3:25; Gal. 3:8.
Aburamu anakwenda Kanaani.
4Ndipo, Aburamu alipoondoka, kama Bwana alivyomwambia, naye Loti akaenda naye. Naye Aburamu alikuwa mwenye miaka 75 alipotoka Harani. 5Aburamu akamchukua mkewe Sarai na Loti, mwana wa nduguye, nayo mapato yao yote, waliyojipatia, nao watu wao wote, waliowapata huko Harani; ndivyo, walivyotoka kwenda katika nchi ya Kanaani. 6Walipofoka katika nchi ya Kanaani, Aburamu akaikata hiyo nchi, mpaka akifika mahali pa Sikemu penye mvule wa More; siku zile Wakanaani walikaa katika nchi hiyo.
Aburamu anatokewa na Bwana.
7Huko Bwana akamtokea Aburamu, akamwambia: Nchi hii nitawapa wao wa uzao wako! Ndipo, alipomjengea Bwana pa kumtambikia, kwa kuwa alimtokea hapo.#1 Mose 13:15; 15:18; 17:8; 24:7; 26:3,4; 28:13; 35:12; 2 Mose 6:4,8; 32:13; Yos. 21:43; Tume. 7:5. 8Kisha akaondoka huko kwenda kwenye mlima ulioko upande wa maawioni kwa jua kwa Beteli, akalipiga hema lake mahali, Beteli ulipokuwa upande wa baharini nao Ai upande wa maawioni kwa jua; huko akajenga pa kumtambikia Bwana, akalitambikia Jina la Bwana.#1 Mose 4:26. 9Kisha Aburamu akaondoka huko, akaendelea kusafiri upande wa kusini.
10Njaa ilipoingia katika nchi ile, Aburamu akashuka kwenda Misri kukaa ugenini huko, kwani njaa ilikuwa kubwa.#1 Mose 20; 26:1-11. 11Walipofika karibu kuingia Misri akamwambia mkewe Sarai: Tazama, ninakujua kuwa mwanamke mwenye mwili mzuri. 12Itakuwa, Wamisri watakapokuona watasema: Huyu ni mkewe. Basi, mimi wataniua, lakini wewe watakuacha, ukae. 13Kwa hiyo sema, ya kuwa u dada yangu, nipate mema kwa ajili yako! Hivyo ndivyo, roho yangu nayo itakavyopona kwa ajili yako. 14Ikawa, Aburamu alipoingia Misri, Wamisri wakamwona mke kuwa mzuri sana. 15Nao wakuu wa Farao walipomwona, wakamsifia Farao; ndipo, huyo mwanamke alipochukuliwa kukaa nyumbani mwa Farao. 16Naye akamfanyia Aburamu mema kwa ajili yake, akapata mbuzi na kondoo na ng'ombe na punda na watumwa wa kiume na wa kike na punda wa kike na ngamia. 17Lakini Bwana akampiga Farao mapigo makuu, nao mlango wake, kwa ajili ya Sarai, mkewe Aburamu.#Sh. 105:14. 18Ndipo, Farao alipomwita Aburamu, akamwambia: Kwa nini umenifanyizia hivyo usiponiambia, ya kuwa ni mkeo? 19Kwa nini umesema: Ni dada yangu, mimi nikamchukua kuwa mke wangu? Sasa mchukue huyu mkeo, uende zako! 20Kisha Farao akamwagizia watu, wampeleke yeye na mkewe na mali zake zote.
Jelenleg kiválasztva:
1 Mose 12: SRB37
Kiemelés
Megosztás
Másolás
Szeretnéd, hogy a kiemeléseid minden eszközödön megjelenjenek? Regisztrálj vagy jelentkezz be
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.