1 Mose 10
10
Vizazi vya Noa.
(Taz. 1 Mambo 1:5-23.)
1Hivi ndivyo vizazi vya wana wa Noa: Semu, Hamu na Yafeti; nao walizaliwa wana baada ya mafuriko ya maji. 2Wana wa Yafeti ni Gomeri na Magogi na Madai na Yawani na Tubali na Meseki na Tirasi. 3Nao wana wa Gomeri ni Askenazi na Rifati na Togarma. 4Nao wana wa Yawani ni Elisa na Tarsisi na Wakiti na Wadodani. 5Kwao hao walijitenga wenyeji wa visiwa vya wamizimu, wakae katika nchi zao, kila kabila lenye msemo wake; hivyo ndivyo, koo zao zilivyopata kuwa mataifa.#Zak. 2:11. 6Nao wana wa Hamu ni Kusi (Nubi) na Misri na Puti na Kanaani. 7Nao wana wa Kusi ni Seba na Hawila na Sabuta na Rama na Sabuteka. Nao wana wa Rama ni Saba na Dedani. 8Kusi akamzaa Nimurodi; ndiye aliyeanza kuwa mwenye nguvu katika nchi. 9Alikuwa mwindaji mwenye nguvu mbele ya Bwana, kwa hiyo watu husema: Mwindaji mwenye nguvu mbele ya Bwana kama Nimurodi. 10Mwanzo wa ufalme wake ulikuwa huko Babeli na Ereki na Akadi na Kalne katika nchi ya Sinari. 11Akatoka katika nchi hii kwenda Asuri, akajenga huko Niniwe na Rehoboti, Iri na Kala,#Yona 1:2. 12tena Reseni katikati ya Niniwe na Kala, nao ni mji mkubwa. 13Naye Misri akawazaa Waludi na Waanami na Walehabi na Wanafutuhi 14na Wapatirusi na Wakasiluhi, ambao Wafilisti walitoka kwao, na Wakafutori. 15Naye Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hiti; 16tna Myebusi na Mwamori na Mgirgasi 17na Mhiwi na Mwarki na Msini, 18na Mwarwadi na Msemari na Mhamati. Halafu koo zao Wakanaani zikasambaa. 19Mipaka yao Wakanaani ilianza Sidoni, ikafika Gerari na Gaza, ikaendelea kufika Sodomu na Gomora na Adima na Seboimu mpaka Lasa. 20Hawa ndio wana wa Hamu, walivyokuwa wenye koo zao na miseo yao, tena ndivyo, mataifa yao walivyokaa katika nchi zao.
21Naye Semu, baba yao wana wote wa Eberi, aliyekuwa kaka yake yafeti, akazaliwa wana.#1 Mose 11:10. 22Wana wa Semu ni Elamu na Asuri na Arpakisadi na Ludi na Aramu. 23Nao wana wa Aramu ni Usi na Huli na Geteri na Masi. 24Naye Arpakisadi akamzaa Sela, naye Sela akamzaa Eberi. 25Naye Eberi akazaliwa wana wawili, jina lake wa kwanza ni Pelegi (Gawanyiko), kwa kuwa siku zake ndipo, nchi hii ilipogawanyika, nalo jina la nduguye ni Yokitani.#1 Mose 11:8. 26Naye Yokitani akamzaa Almodadi na Selefu na Hasarmaweti na Yera, 27na Hadoramu na Uzali na Dikla, 28na Obali na Abimaeli na Saba, 29na Ofiri na Hawila na Yobabu. Hawa wote ndio wana wa Yokitani. 30Nayo makao yao yalianza Mesa, yakafika mpaka mlima wa Sefari ulioko upande wa maawioni kwa jua. 31Hawa ndio wana wa Semu, walivyokuwa wenye koo zao na misemo yao, tena ndivyo, mataifa yao yalivyokaa katika nchi zao.
32Hizi ndizo koo zao wana wa Noa, walivyofuatana kuzaliwa na kugawanyika kuwa mataifa. Kwa hiyo walijitenga kuwa mataifa yaliyokaa katika nchi baada ya mafuriko ya maji.#1 Mose 9:1,19.
Jelenleg kiválasztva:
1 Mose 10: SRB37
Kiemelés
Megosztás
Másolás
Szeretnéd, hogy a kiemeléseid minden eszközödön megjelenjenek? Regisztrálj vagy jelentkezz be
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.