Yohana 11:43-44

Yohana 11:43-44 NENO

Baada ya kusema haya, Isa akapaza sauti yake, akaita, “Lazaro, njoo huku!” Yule aliyekuwa amekufa akatoka nje, mikono yake na miguu yake ikiwa imeviringishiwa vitambaa vya kitani na leso usoni pake. Isa akawaambia, “Mfungueni; mwacheni aende zake.”