Mwanzo 15
15
Agano la Mungu na Abramu
1 #
Mwa 46:2; Isa 41:10; Zab 58:11; 84:11; Ebr 11:6 Baada ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako itakuwa kubwa sana. 2Abramu akasema, Ee Bwana MUNGU, utanipa nini, nami naenda zangu hali sina mtoto, na atakayeimiliki nyumba yangu ni huyu Eliezeri, Mdameski? 3Abramu akasema, Tazama, hukunipa uzao, na mtumwa aliyezaliwa nyumbani mwangu ndiye mrithi wangu.
4 #
Mwa 17:16; 2 Sam 7:12 Nalo neno la BWANA likamjia likinena, Huyu hatakurithi, bali utakayemzaa ndiye atakayekurithi. 5#Rum 4:18; Ebr 11:12; Zab 147:4; Kut 32:13 Akamtoa nje, akasema, Tazama juu mbinguni kisha uzihesabu nyota, kama unaweza kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako. 6#Rum 4:3-6,20-25; Zab 106:31; Gal 3:6; Yak 2:23 Akamwamini BWANA, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki. 7#Mdo 7:2 Kisha akamwambia, Mimi ni BWANA, niliyekuleta kutoka Uru wa Wakaldayo nikupe nchi hii ili uimiliki.
8 #
Amu 6:36-40; 1 Sam 14:9,10; 2 Fal 20:8; Lk 1:18 Akasema, Ee Bwana MUNGU, nipateje kujua ya kwamba nitaimiliki? 9Akamwambia, Unipatie ndama wa miaka mitatu, na mbuzi jike wa miaka mitatu, na kondoo dume wa miaka mitatu, na hua, na mwana njiwa. 10Akampatia hao wote, akawapasua vipande viwili, akaweka kila kipande kuelekea mwenzake, ila ndege hakuwapasua. 11Na tai walipotua juu ya mizoga Abramu akawafukuza. 12#Ayu 4:13,14; Mwa 2:21 Na jua lilipokuwa likichwa usingizi mzito ulimshika Abramu, hofu ya giza kuu ikamwangukia. 13#Kut 1:1-14; 12:40; Mdo 7:6 BWANA akamwambia Abramu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yao, watawatumikia watu wale, nao watateswa kwa muda wa miaka mia nne. 14#Kut 6:6; 7:14; 12:40-41; Mdo 7:7 Hata na taifa lile, watakaowatumikia, nitawahukumu; baadaye watatoka na mali nyingi. 15#Mwa 25:8; Ayu 5:26; Ebr 11:13 Lakini wewe utakwenda kwa baba zako kwa amani, utazikwa katika uzee mwema. 16#Mt 23:32; 1 The 2:16; 2 Pet 3:8,9 Na kizazi cha nne kitarudi hapa, maana uovu wa Waamori haujatimia bado. 17Ikawa, jua lilipokuchwa likawa giza, tazama, tanuri ya moshi na mwenge unaowaka ulipita kati ya vile vipande vya nyama.
18 #
Mdo 7:5; Mwa 17:8; Kum 1:7; Hes 34:3; 2 Nya 9:26; Neh 9:8; Zab 105:11 Siku ile BWANA akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati, 19Mkeni, na Mkenizi, na Mkadmoni, 20na Mhiti, na Mperizi, na Mrefai, 21na Mwamori, na Mkanaani, na Mgirgashi, na Myebusi.
נבחרו כעת:
Mwanzo 15: RSUVDC
הדגשה
שתף
העתק
רוצים לשמור את ההדגשות שלכם בכל המכשירים שלכם? הירשמו או היכנסו
The Holy Bible in Kiswahili, Revised Union Version © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 2013.