Mwanzo 5
5
Wazawa wa Adamu#5:1-32 Nasaba hii ambayo inaweka kiungo kati ya historia ya Adamu na Noa ina majina kumi na mawili. Idadi hiyo kama vile idadi 7 katika Mwa 4:15,18 na 24 huenda inatumiwa kama mfano kwa vile idadi kumi na mbili katika Biblia mara nyingi ni hesabu kamili (rejea k.m. Mwa 24:10; Dan 7:7,20,24; Zek 8:23; Ufu 2:10; 17:3,7, 12,16). Matumizi ya nasaba au orodha ya wazee wa mtu ni jambo linalotajwa mara nyingi katika Biblia kuonesha fulani ni nani na umuhimu wake katika historia. Makabila mbali mbali hata ya huku kwetu Afrika yanatumia sana koo na wazee waliokufa kuonesha umuhimu wa matukio yao. Taz pia nasaba au orodha ya wazee wa Yesu Kristo katika A.J. (Mat 1:1-16; Luka 3:23-38).
(1 Nya 1:1-4)
1Ifuatayo ni orodha ya wazawa wa Adamu. Wakati Mungu alipomuumba binadamu, alimuumba kwa mfano wake. 2Aliwaumba mwanamume na mwanamke, kisha akawabariki#5:2 Akawabariki: Taz Mwa 1:28 maelezo. na kuwapa jina “Binadamu.”
3Adamu alipokuwa na umri wa miaka 130, alipata mtoto aliyefanana naye,#5:3 Aliyefanana naye: Tafsiri ya neno kwa neno ni “kwa sura yake, kwa mfano wake”. Tafsiri nyingine yamkini ni: “aliyefanana naye kabisa”. na mwenye sura kama yake; akamwita Sethi. 4Baada ya kumzaa Sethi, Adamu aliishi miaka 800, na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. 5Adamu alifariki akiwa na umri wa miaka 930.#5:5 Tatizo la umri wa miaka mingi waliyoishi hao watu kumi tangu Adamu mpaka Noa litaendelea kuwa kitendawili.
6Sethi alipokuwa na umri wa miaka 105, alimzaa Enoshi. 7Baada ya kumzaa Enoshi, Sethi aliishi miaka 807, na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. 8Sethi alifariki akiwa na umri wa miaka 912.
9Enoshi alipokuwa na umri wa miaka 90, alimzaa Kenani. 10Baada ya kumzaa Kenani, Enoshi aliishi miaka 815 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. 11Enoshi alifariki akiwa na umri wa miaka 905.
12Kenani alipokuwa na umri wa miaka 70, alimzaa Mahalaleli. 13Baada ya kumzaa Mahalaleli, Kenani aliishi miaka 840 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. 14Kenani alifariki akiwa na umri wa miaka 910.
15Mahalaleli alipokuwa na umri wa miaka 65, alimzaa Yaredi. 16Baada ya kumzaa Yaredi, Mahalaleli aliishi miaka 830 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. 17Mahalaleli alifariki akiwa na umri wa miaka 895.
18Yaredi alipokuwa na umri wa miaka 162, alimzaa Henoki. 19Baada ya kumzaa Henoki, Yaredi aliishi miaka 800 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. 20Yaredi alifariki akiwa na umri wa miaka 962.
21Henoki#5:21 Henoki: Huyu Henoki si sawa na Henoki wa Mwa 4:17. alipokuwa na umri wa miaka 65, alimzaa Methusela. 22Henoki alikuwa mcha Mungu.#5:22,24 Henoki alikuwa mcha Mungu: Katika Kiebrania tuna “Henoki alitembea na Mungu”, yaani katika maisha yake aliiishi kadiri ya matakwa ya Mungu. Katika Mwa 6:9 namna hiyohiyo ya kusema inatumiwa kumtaja Noa kama mtu mwadilifu na mwaminifu kwa Mungu. Baada ya kumzaa Methusela, Henoki aliishi miaka 300 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. 23Henoki aliishi miaka 365.#5:21-23 Umri wa Henoki wa miaka mia tatu sitini na tano huenda ni idadi ya mfano kwa vile mwaka una siku mia tatu sitini na tano. 24Alikuwa mcha Mungu, akatoweka, kwa maana Mungu alimchukua.#5:24 Akatoweka, kwa maana Mungu alimchukua: Katika habari za babu Henoki (aya 21-24) maneno haya yanachukua nafasi ya msemo wa kawaida wa kusema alikufa. Hapa bila shaka kuna maana kwamba Henoki alichukuliwa kutoka duniani kwa kitendo cha pekee cha Mungu hivyo kwamba uhusiano wake wa urafiki na Mungu unaendelea baada ya maisha yake ya hapa duniani. Rejea Ebr 11:5. Taz pia kisa cha Elia katika 2Fal 2:11.
25Wakati Methusela alipokuwa na umri wa miaka 187, alimzaa Lameki. 26Baada ya kumzaa Lameki, Methusela aliishi miaka 782, na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. 27Methusela alifariki akiwa na umri wa miaka 969.
28Wakati Lameki alipokuwa na umri wa miaka 182, alimzaa mtoto wa kiume. 29Alimwita mtoto huyo Noa, akisema, “Mtoto huyu ndiye atakayetufariji#5:29 Noa …ndiye atakayetufariji: Jina Noa lina maana ya “pumziko” na linafanana na kitenzi cha Kiebrania cha neno ambalo lina maana ya “atatufariji”. Tafsiri ya Kigiriki ya Septuajinta (LXX) inatafsiri “atatupa pumziko”. kutokana na kazi yetu ngumu tunayofanya kwa mikono yetu katika ardhi aliyoilaani Mwenyezi-Mungu.” 30Baada ya kumzaa Noa, Lameki aliishi miaka 595 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike. 31Lameki alifariki akiwa na umri wa miaka 777.#5:31 Miaka mia saba sabini na saba: Idadi hiyo yaweza kuwa inatumiwa hapa kama mfano kama hesabu hiyo inavyotumika katika Mwa 4:24.
32Noa alipokuwa na umri wa miaka 500, alimzaa Shemu na Hamu na Yafethi.
Tällä hetkellä valittuna:
Mwanzo 5: BHNTLK
Korostus
Jaa
Kopioi
Haluatko, että korostuksesi tallennetaan kaikille laitteillesi? Rekisteröidy tai kirjaudu sisään
Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993
The Bible Society of Kenya 1993