YouVersion Logo
Search Icon

Zekaria 4

4
Maono ya tano: Kinara cha taa
1Yule malaika aliyeongea nami, akanijia tena, akaniamsha kama kumwamsha mtu usingizini. 2Akaniuliza, “Unaona nini?” Nami nikamjibu, “Ninaona kinara cha taa cha dhahabu. Juu yake kuna bakuli la mafuta na taa saba, na kila moja ina mahali pa kutilia tambi saba. 3Karibu na kinara hicho kuna miti miwili ya mzeituni; mmoja upande wa kulia na mwingine upande wa kushoto.” 4Basi, nikamwuliza huyo malaika, “Bwana, vitu hivi vinamaanisha nini?” 5Naye akanijibu, “Hujui vitu hivi vinamaanisha nini?” Nikamjibu, “Sijui bwana.”#4:5 Vifungu 10b-14: Vimehamishiwa hapa kutoka mwisho wa sura ili kuhifadhi mtiririko wa simulizi. 10bHuyo malaika akaniambia, “Hizo taa saba ni macho saba ya Mwenyezi-Mungu yaonayo kila mahali duniani.” 11Nami nikazidi kuuliza, “Je, hiyo miti miwili ya mizeituni iliyo upande wa kulia na wa kushoto wa kinara, inamaanisha nini? 12Na hayo matawi mawili pembeni mwa mirija miwili ya dhahabu ambamo mafuta ya mizeituni hutiririkia, yanamaanisha nini?” 13Naye akaniambia, “Je, hujui?” Nami nikamjibu, “La, sijui Bwana!” 14Hapo akaniambia, “Matawi haya ndio wale watu wawili waliowekwa wakfu kwa mafuta wamtumikie Bwana wa ulimwengu wote.”
Ahadi ya Mungu kwa Zerubabeli
6Naye akaniambia pia niseme neno hili la Mwenyezi-Mungu kumhusu Zerubabeli: “Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: Huwezi kushinda kwa nguvu au kwa uwezo wako mwenyewe, bali kwa msaada wa roho yangu. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimesema.” 7Tena, akaongeza kusema: “Je, mlima huu ni kizuizi? La! Wewe Zerubabeli utausawazisha. Wewe utaanzisha ujenzi mpya wa hekalu, na wakati utakapoliweka jiwe la mwisho, watu watashangilia wakisema, ‘Ni zuri! Naam, ni zuri!’”
8Neno la Mwenyezi-Mungu likanijia: 9“Zerubabeli ameuweka msingi wa hekalu naye pia atalikamilisha. Hayo yatakapotukia, watu wangu watajua kwamba mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi ndimi niliyekutuma kwao. 10Maendeleo ya ujenzi wa hekalu yanaonekana madogo, na watu wanayadharau; lakini watamwona Zerubabeli akiendelea kulijenga hekalu, nao watafurahi.”

Currently Selected:

Zekaria 4: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy