YouVersion Logo
Search Icon

Gal 5

5
1 # Gal 4:5,31; Mdo 15:10 Katika ungwana huo Kristo alituandika huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa.
Asili ya Uhuru wa Mkristo
2 # 2 Kor 10:1 Tazama, mimi Paulo nawaambia ninyi ya kwamba, mkitahiriwa, Kristo hatawafaidia neno. 3Tena namshuhudia kila mtu atahiriwaye, kwamba ni wajibu wake kuitimiza torati yote. 4Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema. 5Maana sisi kwa Roho tunalitazamia tumaini la haki kwa njia ya imani. 6#Gal 6:15; 1 Kor 7:19Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.
7Mlikuwa mkipiga mbio vizuri; ni nani aliyewazuia msiitii kweli? 8#Gal 1:6Kushawishi huku hakukutoka kwake yeye anayewaita ninyi. 9#1 Kor 5:6Chachu kidogo huchachua donge zima. 10#Gal 1:7; 2 Kor 11:15Nina matumaini kwenu katika Bwana, ya kwamba hamtakuwa na nia ya namna nyingine. Lakini yeye anayewafadhaisha atachukua hukumu yake, awaye yote. 11#1 Kor 1:23Nami, ndugu zangu ikiwa ninahubiri habari ya kutahiriwa, kwa nini ningali ninaudhiwa? Hapo kwazo la msalaba limebatilika! 12#Zab 12:3Laiti hao wanaowatia mashaka wangejikata nafsi zao!
13 # 1 Pet 2:16 Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo. 14#Law 19:18Maana torati yote imetimilika katika neno moja, nalo ni hili, Umpende jirani yako kama nafsi yako. 15Lakini mkiumana na kulana, angalieni msije mkaangamizana.
Kazi za Kimwili
16Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. 17#Rum 7:15-23; Yak 4:5; 1 Pet 2:11Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. 18#Rum 8:14Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria. 19#1 Kor 6:9,10Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, 20ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, 21#Efe 5:5; Ufu 22:15husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
Tunda la Roho
22 # Efe 5:9 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, 23#1 Tim 1:9upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. 24#Rum 6:6; Kol 3:5; 1 Pet 2:11Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. 25#Rum 8:4Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho. 26#Flp 2:3Tusijisifu bure, tukichokozana na kuhusudiana.

Currently Selected:

Gal 5: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy