Efe UTANGULIZI
UTANGULIZI
Paulo aliandika waraka huu pamoja na nyaraka kwa Wafilipi, Wakolosai, na Filemoni akiwa kifungoni kule Rumi (Mdo 28:16, 30; Efe 3:1; 4:1; 6:20). Nyaraka hizi huitwa “Nyaraka za Kifungoni” (Flp 1:7,12-17; Kol 4:3,10,18; Flm 1:9-10).
Waraka huu unaadhimisha au kueleza sifa za uhai wa kanisa ambalo ni jumuiya ya pekee iliyoanzishwa na Mungu kwa njia ya Yesu Kristo. Hivyo basi Yesu ndiye kichwa cha kanisa na cha ulimwengu wote ulioumbwa na Mungu. Kanisa lilianzishwa kwa kuzingatia malengo ya milele ya Mungu, na ndani ya kanisa waumini wanaishi katika muungano na Mungu kwa njia ya Kristo na Roho Mtakatifu, hali ambayo ni matarajio ya muungano kamili katika maisha yajayo. Hiyo ndiyo picha maalumu tunayopewa kwa jumla katika waraka huu wa pekee.
Paulo aliandika Waraka huu ukapelekwa na Tikiko kule Efeso na makanisa ya maeneo hayo (6:21-22; Kol 4:7) ili kuimarisha imani yao. Kwa kifo cha Yesu Kristo watu wamepatanishwa na Mungu, nguvu za yule mwovu zikavunjwa na mfarakano uliokuwako kati ya Wayahudi na wasio Wayahudi ukaondolewa. Kwa sababu hiyo Paulo anawaonya Wakristo wasio Wayahudi na wale wa Kiyahudi wasidharauliane na kutengana bali washirikiane na kuwa na umoja. Kristo aliondoa kile kilichowatenganisha kati yao na Mungu, na wao kwa wao. Kristo amewaunganisha na Mungu, akawafanya wapya na kuwapa maisha mapya. Paulo anatilia mkazo umoja wa kanisa pamoja na mwenendo mpya wa kikristo.
Currently Selected:
Efe UTANGULIZI: SUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.