Yohana MT. 2
2
1NA siku ya tatu palikuwa arusi katika Kana ya Galilaya, na mama yake Yesu alikuwako. 2Yesu nae akaitwa pamoja na wanafunzi wake arusini. 3Hatta divai ilipowatindikia, mama yake Yesu akamwambia, Hawana divai. 4Yesu akamwambia, Bibi, ina nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia. 5Mama yake akawaambia watumishi, Lo lote atakalowaambieni fanyeni. 6Palikuwako mabalasi sita ya mawe, yamewekwa huko kwa desturi ya kutawaza kwao Wayahudi, killa moja lapata kadiri ya nzio mbili au tatu. 7Yesu akawaambia, Jalizeni mabalasi maji. Wakayajaliza hatta juu. 8Akawaambia, Sasa tekeni, mpelekeeni mkuu wa meza. Wakapeleka. 9Mkuu wa meza alipoyaonja maji yaliyofanyika kuwa divai, asijue ilikotoka, (lakini watumishi walijua walioyateka maji), mkuu wa meza akamwita bwana arusi, 10akamwambia, Killa mtu kwanza huandaa divai iliyo njema, hatta watu wakiisha kunywa sana, ndipo huleta iliyo dhaifu: wewe umeweka divai iliyo njema hatta sasa. 11Mwanzo huu wa ishara Yesu alifanya Kana ya Galilaya, akauonyesha utukufu wake, wanafunzi wake wakamwamini.
12Baada ya haya akashuka hatta Kapernaum, yeye na mama yake na ndugu zake na wanafunzi wake: wakakaa huko siku chache. 13Na Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu: Yesu akapanda hatta Yerusalemi. 14Akaona hekaluni watu waliokuwa wakiuza ngʼombe na kondoo na njiwa, na wenye kuvunja fedha wameketi; 15Akafanya mjeledi kwa kambaa akawatoa wote katika hekalu, na kondoo, na ngʼombe, akamwaga fedha yao wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao; 16akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoem haya: msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara. 17Wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa imeandikwa, Wivu wa nyumba yako umenila. 18Bassi Wayahudi wakajibu wakamwambia, Ishara gani utuonyeshayo, iwapo unafanya haya? 19Yesu akajibu, akawaambia, Livunjeni hekalu hii, nami kwa siku tatu nitaisimamisha. 20Bassi Wayahudi wakasema, Hekalu hii ilijengwa katika muda wa miaka arubaini na sita, nawe utaisimamisha kwa siku tatu? 21Lakini yeye alinena khabari za hekalu ya mwili wake. 22Bassi alipofufuliwa katika wafu, wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa amenena neno hili, wakaliamini lile andiko na lile neno alilolinena Yesu.
23Hatta alipokuwapo Yerusalemi wakati wa Pasaka katika siku kuu, watu wengi wakaliamini jina lake, wakiona ishara zake alizozifanya. 24Lakini Yesu hakujiaminisha kwao, kwa kuwa yeye aliwajua wote; 25na kwa sababu hakuwa na haja ya watu kushuhudia khabari za niwana Adamu; kwa maana yeye mwenyewe alijua yaliyomo ndani ya mwana Adamu.
Zur Zeit ausgewählt:
Yohana MT. 2: SWZZB1921
Markierung
Teilen
Kopieren
Möchtest du deine gespeicherten Markierungen auf allen deinen Geräten sehen? Erstelle ein kostenloses Konto oder melde dich an.
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.