Lk 22
22
Mpango wa Kumwua Yesu
1 #
Mt 26:1-5; Mk 14:1,2 Ikakaribia sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, iitwayo Sikukuu ya Pasaka. 2#Lk 20:19Na wakuu wa makuhani na waandishi walikuwa wakitafuta njia ya kumwua; maana walikuwa wakiwaogopa watu.
3 #
Mt 26:14-16; Mk 14:10,11 #
Yn 13:2,27 Shetani akamwingia Yuda, aitwaye Iskariote, naye ni mmoja wa wale Thenashara. 4Akaondoka, akaenda akasema na wakuu wa makuhani na majemadari, jinsi atakavyoweza kumtia mikononi mwao. 5Wakafurahi, wakapatana naye kumpa fedha. 6Akakubali, akatafuta nafasi ya kumsaliti kwao pasipokuwapo mkutano.
Maandalizi ya Pasaka
7 #
Mt 26:17-29; Mk 14:12-25 #
Kut 12:18-20
Ikafika siku ya mikate isiyotiwa chachu, ambayo ilipasa kuchinja pasaka. 8Akawatuma Petro na Yohana, akisema, Nendeni, mkatuandalie pasaka tupate kuila. 9Wakamwambia, Wataka tuandae wapi? 10Akawaambia, Tazama, mtakapoingia mjini mtakutana na mwanamume akichukua mtungi wa maji; mfuateni mkaingie katika nyumba atakayoingia yeye. 11Na mtamwambia mwenye nyumba, Mwalimu akuambia, Ki wapi chumba cha wageni, nipate kula pasaka humo pamoja na wanafunzi wangu? 12Naye atawaonyesha chumba kikubwa orofani, kimekwisha andikwa; andaeni humo. 13#Lk 19:32Wakaenda, wakaona kama alivyowaambia, wakaiandaa pasaka.
Kuanzishwa kwa Chakula cha Bwana
14Hata saa ilipofika aliketi chakulani, yeye na wale mitume pamoja naye. 15Akawaambia, Nimetamani sana kuila pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu; 16#Lk 13:29kwa maana nawaambia ya kwamba siili tena hata itakapotimizwa katika ufalme wa Mungu. 17Akapokea kikombe, akashukuru, akasema, Twaeni hiki, mgawanye ninyi kwa ninyi; 18Maana nawaambia ya kwamba tangu sasa sinywi mazao ya mzabibu hata ufalme wa Mungu utakapokuja. 19#1 Kor 11:23-25; Mdo 27:35Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, [Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. 20#Kut 24:8; Yer 31:31; Zek 9:11Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.] 21#Yn 13:21,22Walakini, tazama, mkono wake yeye anayenisaliti upo hapa pamoja nami mezani, 22Kwa kuwa Mwana wa Adamu aenda zake kama ilivyokusudiwa; lakini, ole wake mtu yule amsalitiye! 23Wakaanza kuulizana wao kwa wao, ni yupi miongoni mwao atakayelitenda jambo hilo.
Mashindano kuhusu Ukubwa
24 #
Mt 18:1; Mk 9:34; Lk 9:46 Yakatokea mashindano kati yao, kwamba ni nani anayehesabiwa kuwa mkubwa. 25#Mt 20:25-27; Mk 10:42-44Akawaambia, Wafalme wa Mataifa huwatawala, na wenye mamlaka juu yao huitwa Wenye fadhili; 26#Mt 23:11; Mk 9:35lakini kwenu ninyi sivyo; bali aliye mkubwa kwenu na awe kama aliye mdogo; na mwenye kuongoza kama yule atumikaye. 27#Yn 13:12-15Maana aliye mkubwa ni yupi? Yeye aketiye chakulani, au yule atumikaye? Siye yule aketiye chakulani? Lakini mimi kati yenu ni kama atumikaye. 28Nanyi ndinyi mliodumu pamoja nami katika majaribu yangu. 29#Lk 12:32Nami nawawekea ninyi ufalme, kama vile Baba yangu alivyoniwekea mimi; 30#Mt 19:28mpate kula na kunywa mezani pangu katika ufalme wangu; na kuketi katika viti vya enzi, huku mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli.
Yesu Atabiri kuhusu Petro Kumkana
31 #
Mt 26:31-35; Mk 14:27-31; Yn 13:36-38 #
2 Kor 2:11; Amo 9:9 Akasema, Simoni, Simoni, tazama, Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano; 32#Yn 17:11,15,20; Zab 51:13lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike; nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako. 33Akamwambia, Bwana, niwapo pamoja nawe, mimi ni tayari kwenda gerezani au hata kifoni. 34Akasema, Nakuambia, Petro, jogoo hatawika leo, kabla wewe hujanikana mara tatu ya kuwa hunijui.
Mfuko, Mkoba, na Upanga
35 #
Mt 10:9-10; Mk 6:8-9; Lk 9:3; 10:4 Akawauliza, Je! Hapo nilipowatuma hamna mfuko, wala mkoba, wala viatu, mlipungukiwa na kitu? Wakasema, La! 36Akawaambia, Lakini sasa mwenye mfuko na auchukue, na mkoba vivyo hivyo; naye asiye na upanga, na auze joho yake akanunue. 37#Isa 53:12; Lk 22:52Kwa kuwa nawaambia, hayo yaliyoandikwa hayana budi kutimizwa kwangu; ya kuwa, Alihesabiwa pamoja na wahalifu. Kwa sababu yanipasayo yanao mwisho wake. 38Wakasema, Bwana, tazama, hapa pana panga mbili. Akawaambia, Basi.
Yesu Aomba katika Mlima wa Mizeituni
39 #
Mt 26:30,36-46; Mk 14:26,32-42 #
Lk 21:37; Yn 18:1 Akatoka akaenda mpaka mlima wa Mizeituni kama ilivyokuwa desturi yake; wanafunzi wake nao wakafuatana naye.
40Alipofika mahali pale aliwaambia, Ombeni kwamba msiingie majaribuni. 41Mwenyewe akajitenga nao kama kiasi cha kutupa jiwe, akapiga magoti akaomba, 42#Mt 6:10akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke. [ 43#1 Fal 19:5; Yn 12:29Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu. 44Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini.] 45Alipoondoka katika kuomba kwake, akawajia wanafunzi wake, akawakuta wamelala usingizi kwa huzuni. 46Akawaambia, Mbona mmelala usingizi? Ondokeni, mkaombe, msije mkaingia majaribuni.
Kusalitiwa na Kukamatwa kwa Yesu
47 #
Mt 26:47-56; Mk 14:43-49; Yn 18:2-11 Basi alipokuwa katika kusema, tazama, mkutano wa watu, na yule aitwaye Yuda, ambaye ni mmoja wa wale Thenashara, amewatangulia. Akamkaribia Yesu ili kumbusu. 48Yesu akamwambia, Yuda, wamsaliti Mwana wa Adamu kwa kumbusu? 49Na wale waliokuwa karibu naye walipoona yatakayotukia, walisema, Bwana, tuwapige kwa upanga? 50Mmoja wao akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio la kuume. 51Yesu akajibu akasema, Mwe radhi kwa hili. Akamgusa sikio, akamponya. 52#Lk 22:37Yesu akawaambia wakuu wa makuhani, na maakida wa hekalu, na wazee, waliokuja juu yake, Je! Mmekuja wenye panga na marungu kama kukamata mnyang’anyi? 53#Lk 19:47; 21:37; Yn 7:30; 8:20; Kol 1:13Kila siku nilipokuwa pamoja nanyi hekaluni hamkuninyoshea mikono, lakini hii ndiyo saa yenu, na mamlaka ya giza.
Petro Amkana Yesu
54 #
Mt 26:57,58,69-75; Mk 14:53,54,66-72; Yn 18:12-18,25-27 Wakamkamata, wakamchukua, wakaenda naye nyumbani kwa Kuhani Mkuu. Na Petro alimfuata kwa mbali. 55Na walipokwisha washa moto katikati ya kiwanja, waliketi pamoja, naye Petro akaketi kati yao. 56Ndipo mjakazi mmoja akamwona ameketi mwangani, akamkazia macho akasema, Na huyu alikuwa pamoja naye. 57Akakana, akisema, Ee mwanamke, simjui. 58Baadaye kitambo mtu mwingine alimwona akasema, Wewe nawe u mmoja wao. Petro akasema, Ee mtu, si mimi. 59Halafu, yapata saa moja, mtu mwingine alikaza kusema, Hakika na huyu alikuwa pamoja naye, kwa kuwa yeye pia ni Mgalilaya. 60Petro akasema, Ee mtu, sijui usemalo. Na papo hapo alipokuwa katika kusema, jogoo aliwika. 61#Lk 22:34Bwana akageuka akamtazama Petro. Petro akalikumbuka lile neno la Bwana jinsi alivyomwambia, Leo kabla hajawika jogoo utanikana mara tatu. 62Akatoka nje akalia kwa majonzi.
Kumdhihaki na Kumpiga Yesu
63 #
Mt 26:67,68; Mk 14:65 Na wale watu waliokuwa wakimshika Yesu walimfanyia dhihaka, wakampiga. 64Wakamfunika macho, kisha wakamwuliza-uliza wakisema, Tabiri, ni nani aliyekupiga? 65Wakamtolea na maneno mengine mengi ya kumtukana.
Yesu Mbele ya Baraza
66 #
Mt 26:59-66; Mk 14:55-64 Hata kulipokucha, walikutanika jamii ya wazee, na wakuu wa makuhani, na waandishi, wakamleta katika baraza yao, wakisema, 67#Yn 3:12; 8:45; 10:24Kama wewe ndiwe Kristo, tuambie. Akawaambia, Nijapowaambia, hamtasadiki kabisa. 68Tena, nikiwauliza, hamtajibu. 69#Dan 7:13; Zab 110:1Lakini tangu sasa Mwana wa Adamu atakuwa ameketi upande wa kuume wa Mungu Mwenyezi. 70Wakasema wote, Basi, wewe ndiwe Mwana wa Mungu? Akawaambia, Ninyi mwasema kwamba mimi ndiye. 71Wakasema, Basi, tuna haja gani tena ya ushuhuda? Maana, sisi wenyewe tumesikia maneno ya kinywa chake.
Dewis Presennol:
Lk 22: SUV
Uwcholeuo
Rhanna
Copi
Eisiau i'th uchafbwyntiau gael eu cadw ar draws dy holl ddyfeisiau? Cofrestra neu mewngofnoda
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.