Logo YouVersion
Eicon Chwilio

Yn 15

15
Yesu ni Mzabibu wa Kweli
1 # Yer 2:21; Zab 80:8 Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima. 2#Mt 15:13Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa. 3Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia. 4Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. 5#1 Kor 12:12,27; 2 Kor 3:5Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote. 6#Mt 3:10; 13:40Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea. 7#Mk 11:24Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa. 8#Mt 5:16Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.
9Kama vile Baba alivyonipenda mimi, nami nilivyowapenda ninyi, kaeni katika pendo langu. 10#Yn 8:29; 14:15; 1 Yoh 2:4,8Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake. 11#Yn 17:13Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe. 12#Yn 13:34; 15:17; 1 Yoh 3:11,23; 2 Yoh 1:5; Mk 12:30Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi. 13#Yn 10:12; 1 Yoh 3:16Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. 14#Yn 8:31; Mt 12:50; 28:20Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo. 15Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu. 16#Yn 6:70; 13:18Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni. 17Haya nawaamuru ninyi, mpate kupendana.
Chuki ya Ulimwengu
18 # Yn 7:7; 1 Yoh 3:13 Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi. 19#1 Yoh 4:5; Yn 17:14; Lk 6:22Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia. 20#Mt 10:24; Lk 6:40; Yn 13:16Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu. 21#Yn 10:22; 16:3; Mt 5:11; Mk 13:13Lakini haya yote watawatenda kwa ajili ya jina langu, kwa kuwa hawamjui yeye aliyenipeleka. 22Kama nisingalikuja na kusema nao, wasingalikuwa na dhambi; lakini sasa hawana udhuru kwa dhambi yao. 23#Yn 5:23; 1 Yoh 2:23; Lk 10:16Yeye anichukiaye mimi humchukia na Baba yangu. 24#Yn 14:11Kama nisingalitenda kwao kazi asizozitenda mtu mwingine, wasingalikuwa na dhambi; lakini sasa wametuona mimi na Baba yangu, na kutuchukia. 25#Zab 35:19; 69:4Lakini litimie lile neno lililoandikwa katika torati yao, Walinichukia bure. 26#Yn 14:26; Lk 24:49Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia. 27#Lk 1:2; Mdo 1:8; 5:32Nanyi pia mnashuhudia, kwa kuwa tangu mwanzo mmekuwapo pamoja nami.

Dewis Presennol:

Yn 15: SUV

Uwcholeuo

Rhanna

Copi

None

Eisiau i'th uchafbwyntiau gael eu cadw ar draws dy holl ddyfeisiau? Cofrestra neu mewngofnoda