Logo YouVersion
Eicon Chwilio

Yn 1

1
Neno akawa Mwili
1 # 1 Yoh 1:1,2; Yn 17:5; Ufu 19:13 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. 2#Mit 8:22Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu. 3#Kol 1:16,17; Ebr 1:2Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. 4#Yn 5:26Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. 5#Yn 3:19Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza.
6 # Mt 3:1; Mk 1:4; Lk 3:1-2; 1:13-17,57-80 Palitokea mtu, ametumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana. 7#Lk 3:3Huyo alikuja kwa ushuhuda, ili aishuhudie ile nuru, wote wapate kuamini kwa yeye. 8#Yn 1:20Huyo hakuwa ile nuru, bali alikuja ili aishuhudie ile nuru. 9Kulikuwako Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu. 10#Yn 1:3-5Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua. 11Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea. 12#Gal 3:26Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; 13#Yn 3:5,6waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu. 14#Isa 7:14; 2 Pet 1:16,17; Isa 60:1; Lk 9:32Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
15 # Yn 1:27,30; Mt 3:11 Yohana alimshuhudia, akapaza sauti yake akasema, Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Ajaye nyuma yangu amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu. 16#Yn 3:34; Kol 1:19Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema. 17#Rum 6:14; 10:4; Kut 34:6; Zab 25:10; 40:10; 85:10Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo. 18#Yn 6:46; 1 Yoh 4:12; Mt 11:27; Lk 10:22; 1 Tim 6:16Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua.
Ushuhuda wa Yohana Mbatizaji
19 # Lk 3:15,16 Na huu ndio ushuhuda wake Yohana, Wayahudi walipotuma kwake makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu ili wamwulize, Wewe u nani? 20#Mdo 13:25Naye alikiri, wala hakukana; alikiri kwamba, Mimi siye Kristo. 21#Kum 18:15,18; Mal 4:5; Mt 17:10; Yn 6:14; 7:40Wakamwuliza, Ni nini basi? U Eliya wewe? Akasema, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La. 22Basi wakamwambia, U nani? Tuwape majibu wale waliotupeleka. Wanenaje juu ya nafsi yako? 23#Isa 40:3; Mt 3:3; Mk 1:3; Lk 3:4Akasema, Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, Inyosheni njia ya Bwana! Kama vile alivyonena nabii Isaya. 24Nao wale waliotumwa walikuwa wametoka kwa Mafarisayo. 25#Mt 21:25Wakamwuliza, wakamwambia, Mbona basi wabatiza, ikiwa wewe si Kristo, wala Eliya, wala nabii yule? 26#Mt 3:11; Mk 1:7,8Yohana akawajibu akisema, Mimi nabatiza kwa maji. Katikati yenu amesimama yeye msiyemjua ninyi. 27#Yn 3:26; Mdo 13:25Ndiye yule ajaye nyuma yangu, ambaye mimi sistahili kuilegeza gidamu ya kiatu chake. 28#Mt 3:6,13Hayo yalifanyika huko Bethania ng’ambo ya Yordani, alikokuwako Yohana akibatiza.
Mwanakondoo wa Mungu
29 # Yn 1:36; Isa 53:7 Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu! 30#Yn 15:27Huyu ndiye niliyenena habari zake ya kwamba, Yuaja mtu nyuma yangu, ambaye amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu. 31Wala mimi sikumjua; lakini kusudi adhihirishwe kwa Israeli ndiyo maana mimi nalikuja nikibatiza kwa maji. 32#Mt 3:16; Mk 1:10; Lk 3:22Tena Yohana akashuhudia akisema, Nimemwona Roho akishuka kama hua kutoka mbinguni; naye akakaa juu yake. 33#Lk 3:2; Mt 3:16Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu. 34#Mt 3:17Nami nimeona, tena nimeshuhudia ya kuwa huyu ni Mwana wa Mungu.
Wanafunzi wa kwanza wa Yesu
35Tena siku ya pili yake Yohana alikuwa amesimama pamoja na wawili katika wanafunzi wake. 36#Yn 1:29; Isa 53:7Akamtazama Yesu akitembea, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu! 37Wale wanafunzi wawili wakamsikia akinena, wakamfuata Yesu. 38Yesu aligeuka, akawaona wakimfuata, akawaambia, Mnatafuta nini? Wakamwambia, Rabi, (maana yake, Mwalimu), unakaa wapi? 39Akawaambia, Njoni, nanyi mtaona. Wakaenda, wakaona akaapo, wakakaa kwake siku ile. Nayo ilikuwa yapata saa kumi. 40#Mt 4:18-22Andrea, nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohana na kumfuata Yesu. 41#1 Sam 2:10; Zab 2:2Huyo akamwona kwanza Simoni, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake, Kristo). 42#Mt 16:18; Mk 3:16Akampeleka kwa Yesu. Naye Yesu akamtazama, akasema, Wewe u Simoni, mwana wa Yohana; nawe utaitwa Kefa (tafsiri yake Petro, au Jiwe).
Yesu Awaita Filipo na Nathanaeli
43 # Mt 8:22; Mk 2:14 Siku ya pili yake alitaka kuondoka kwenda Galilaya, naye akamwona Filipo. Yesu akamwambia, Nifuate. 44Naye Filipo alikuwa mtu wa Bethsaida, mwenyeji wa mji wa Andrea na Petro. 45#Kum 18:18; Isa 7:14; 53:2; Yer 23:5; Eze 34:23Filipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na manabii, Yesu, mwana wa Yusufu, mtu wa Nazareti. 46#Yn 7:41,52Nathanaeli akamwambia, Laweza neno jema kutoka Nazareti? Filipo akamwambia, Njoo uone. 47#Zab 32:2; 73:1; Mwa 25:27Basi Yesu akamwona Nathanaeli anakuja kwake, akanena habari zake, Tazama, Mwisraeli kweli kweli, hamna hila ndani yake. 48Nathanaeli akamwambia, Umepataje kunitambua? Yesu akajibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona. 49#2 Sam 7:14; Yn 6:69; Zab 2:7; Mt 14:33; 16:16Nathanaeli akamjibu, Rabi, wewe u Mwana wa Mungu, ndiwe Mfalme wa Israeli. 50Yesu akajibu, akamwambia, Kwa sababu nilikuambia, Nilikuona chini ya mtini, waamini? Utaona mambo makubwa kuliko haya. 51#Mwa 28:12; Mt 4:11; Mk 1:13Akamwambia, Amin, amin, nawaambia, Mtaziona mbingu zimefunguka na malaika wa Mungu wakikwea na kushuka juu ya Mwana wa Adamu.

Dewis Presennol:

Yn 1: SUV

Uwcholeuo

Rhanna

Copi

None

Eisiau i'th uchafbwyntiau gael eu cadw ar draws dy holl ddyfeisiau? Cofrestra neu mewngofnoda