YouVersion Logo
Search Icon

Yobu 4

4
Hoja ya Elifazi
(4:1–14:22)
1Kisha Elifazi yule Mtemani akamjibu Yobu:
2“Je, mtu akijaribu kukuambia neno utakasirika?
Lakini nani awezaye kujizuia kusema?
3Sikiliza! Wewe umewafundisha wengi,
na kuiimarisha mikono ya wanyonge.
4Maneno yako yamewainua waliokufa moyo,
umewaimarisha waliokosa nguvu.
5Lakini sasa yamekupata, nawe ukakosa subira,
yamekugusa, nawe ukafadhaika.
6Je, kumcha Mungu si ndilo tegemeo lako?
Na unyofu wako si ndilo tumaini lako?
7Fikiri sasa: Nani asiye na hatia ambaye amepata kuangamia?
Au, je, waadilifu wamepata kutupwa?
8Nijuavyo mimi, wapandao uovu na ubaya huvuna hayohayo,
9Mungu huwaangamiza hao kwa pumzi yake,
hao huteketezwa kwa pigo la hasira yake.
10Waovu hunguruma kama simba mkali,
lakini meno yao huvunjwa.
11Simba mwenye nguvu hufa kwa kukosa mawindo,
na watoto wa simba jike hutawanywa!
12“Siku moja, niliambiwa neno kwa siri,
sikio langu lilisikia mnongono wake.
13 # Taz Yobu 33:15 Nikiwa katika mawazo ya njozi za usiku,
wakati usingizi mzito huwashika watu,
14nilishikwa na hofu na kutetemeka,
mifupa yangu yote ikagonganagongana.
15Upepo ukapita mbele ya uso wangu,
nywele za mwilini mwangu zikajisimamisha.
16Kitu kilisimama tuli mbele yangu,
nilipokitazama sikukitambua kabisa.
Kulikuwa na umbo fulani mbele yangu;
kulikuwa kimya, kisha nikasikia sauti.
17Binadamu afaye aweza kuwa mwadilifu mbele ya#4:17 mbele ya: Au kuliko Mungu?
Mtu aweza kuwa safi mbele ya Muumba wake?
18Hata watumishi wake, Mungu hana imani nao;
na malaika wake huwaona wana kosa;
19sembuse binadamu viumbe vya udongo,
watu ambao chanzo chao ni mavumbi,
ambao waweza kupondwapondwa kama nondo!
20Binadamu kwa masaa machache tu waweza kuangamia;
huangamia milele bila kuacha hata alama yao!
21Iwapo uzi unaoshikilia uhai wao ukikatwa
wao hufa tena bila kuwa na hekima.

Currently Selected:

Yobu 4: BHN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in

YouVersion uses cookies to personalize your experience. By using our website, you accept our use of cookies as described in our Privacy Policy