3 Yohane UTANGULIZI
UTANGULIZI
Barua hii ya tatu ya Yohane, kama ile ya pili, ni fupi sana. Hata hapa mwandishi anajitaja kama “Mzee” (taz 2 Yohane) na anayeandikiwa anatajwa kama Gayo ambaye ni rafiki wa pekee wa mwandishi. Hatujui chochote kuhusu huyu Gayo isipokuwa tu kwamba alikuwa mwaamini na alikuwa imara katika kumwamini Kristo. Habari tunayoambiwa juu yake ni kinyume kabisa cha habari za mtu mwingine anayetajwa katika barua hii yaani Diotrefe. Huyu bila shaka alikuwa mtu mashuhuri katika jumuiya ya Wakristo ambaye alimpuuza huyo “Mzee” na kukosa ukarimu.
Mwandishi anamsifu Gayo kwa uaminifu na utumishi wake (taz 1-8); anashutumu mwenendo wa Diotrefe (taz 9-10), kisha anataja tabia njema ya mwaamini mwingine aitwaye Demetrio (11-12) na kumalizia kwa kuzungumzia ziara yake ya kulitembelea hilo kanisa, na mwishoni salamu za mwisho (12-15).
Currently Selected:
3 Yohane UTANGULIZI: BHN
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (Yenye Vitabu vya Deuterokanoni): Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa (BHN): Hakimiliki -1995, 2001: kwa Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.