2 Yohane UTANGULIZI
UTANGULIZI
Mwandishi wa barua hii anajiita “Mzee” na ni dhahiri jina hili latumiwa kuonesha kwamba mwandishi aliheshimika katika jumuiya. Na anayeandikiwa anatajwa kama “Bimkubwa mteule, pamoja na watoto wako” maneno ambayo bila shaka yanatumika hapa kwa mfano wa jumuiya ya kanisa la mahali fulani (1:1).
Barua yenyewe yawatia moyo wasomaji wake waishi kwa kuzingatia ukweli na upendo; hayo mawili yamaanisha kuwa waumini wanapaswa kushika amri za Mungu. Barua hii pia inawaonya wasomaji wake wawe na tahadhari juu ya mafundisho ya uongo, jambo ambalo lilitajwa pia katika barua ya kwanza. Na kama vile katika barua ile ya kwanza, mwandishi anawahimiza waumini wawe waangalifu na kudumu katika imani ya kweli.
Currently Selected:
2 Yohane UTANGULIZI: BHN
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (Yenye Vitabu vya Deuterokanoni): Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa (BHN): Hakimiliki -1995, 2001: kwa Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.