Yobu 42
42
1Kisha Yobu akamjibu Mwenyezi-Mungu:
2“Najua kwamba waweza kila kitu,
lolote unalokusudia haliwezi kuzuiliwa.
3 # Taz Yobu 38:2 Ulisema kuwa nilithubutu kutatiza mpango wako kijinga.
Kweli nilitamka kitu ambacho sikuelewa
mambo ya ajabu mno kwangu
ambayo sikuwa ninayajua.
4 # Taz Yobu 38:3 Uliniambia nisikilize nawe utaniambia;
kwamba utaniuliza nami nikujibu.
5Kweli nilikuwa nimesikia habari zako kwa masikio tu,
lakini sasa nakuona kwa macho yangu mwenyewe.
6Kwa hiyo natubu pamoja na kujipaka mavumbi na majivu,
najiona mimi mwenyewe kuwa si kitu kabisa.”
Hatima
7Mwenyezi-Mungu alipomaliza kuongea na Yobu, alimwambia Elifazi, Mtemani, “Ghadhabu yangu imewaka dhidi yako na marafiki zako wawili kwani hamkusema ukweli juu yangu kama mtumishi wangu Yobu alivyofanya. 8Kwa hiyo chukueni mafahali saba na kondoo madume saba, mwende kwa mtumishi wangu Yobu, mkawatoe sadaka ya kuteketezwa kwa ajili yenu. Naye mtumishi wangu Yobu atawaombeeni, nami nitaisikiliza sala yake na kuacha kuwatenda kulingana na upumbavu wenu; maana hamkusema ukweli juu yangu kama mtumishi wangu Yobu alivyofanya.”
9Basi, Elifazi Mtemani, Bildadi, Mshua na Sofari Mnaamathi, wakafanya kama Mwenyezi-Mungu alivyowaambia. Mwenyezi-Mungu akaipokea sala ya Yobu.
10 # Taz Yobu 1:1-3 Baada ya Yobu kuwaombea rafiki zake, Mwenyezi-Mungu akamrudishia Yobu hali yake ya kwanza. Alimpa maradufu ya yote aliyokuwa nayo hapo awali. 11Kisha ndugu zake, dada zake na rafiki wote waliomfahamu hapo awali wakamwendea nyumbani kwake, wakala chakula pamoja naye. Wakampa pole na kumfariji kwa ajili ya mateso yote ambayo Mwenyezi-Mungu alikuwa amemletea. Kila mmoja wao akampa Yobu fedha na pete ya dhahabu.
12Katika miaka ya Yobu iliyofuata Mwenyezi-Mungu alimbariki zaidi kuliko hata alivyokuwa amembariki pale awali. Basi Yobu akawa na kondoo 14,000, ngamia 6,000, ng'ombe 2,000 na punda majike 1,000. 13Alikuwa pia na watoto wa kiume saba na wa kike watatu. 14Binti yake wa kwanza alimpa jina Yemima, wa pili Kezia, na wa mwisho Keren-hapuki.#42:14 Yemima: Maana yake: Njiwa. 15Katika nchi yote hiyo hapakuwa na wanawake waliokuwa wazuri kama mabinti wa Yobu. Baba yao akawaachia urithi kama alivyowaachia kaka zao.
16Baada ya hapo, Yobu aliishi miaka 140, akawaona wajukuu na vitukuu vyake vyote hadi kizazi cha nne. 17Basi, Yobu akafariki akiwa mzee wa miaka mingi.
Currently Selected:
Yobu 42: BHND
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (Yenye Vitabu vya Deuterokanoni): Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa (BHN): Hakimiliki -1995, 2001: kwa Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Learn More About Biblia Habari Njema