YouVersion Logo
Search Icon

Mattayo MT. 8

8
1ALIPOSHUKA mlimani, makutano mengi walimfuata. 2Akaja mwenye ukoma akamsujudu, akinena, Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa. 3Yesu akanyosha mkono wake, akamgusa, akinena, Nataka: takasika. Marra ukoma wake ukatakasika. 4Yesu akamwambia, Angalia, usimwambie mtu; illa enenda zako, ukajionyeshe kwa kuhani, utoe sadaka kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwao.
5Hatta Yesu alipoingia Kapernaum, akida alimjia, akamsihi, 6akinena, Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana. 7Yesu akamwambia. Nitakuja, nimponye. 8Akida akamjibu, akasema, Si stahili yangu wewe uingie chini ya dari yangu: lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona. 9Maana na mimi ni mtu chini ya mamlaka, nina askari chini yangu: nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; au mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya. 10Yesu aliposikia haya, akastaajabu, akawaambia wale waliomfuata, Amin, nawaambieni, Sijaona imani kubwa kama hii, hatta katika Israeli. 11Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magbaribi, wataketi pamoja na Ibrabimu, na Isaak, na Yakob katika ufalme wa mbinguni; 12bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje; ndiko kutakuwa kilio na kusaga meno. 13Yesu akamwambia akida, Nenda zako: na kadiri ulivyoamini upate. Mtumishi wake akapona saa ileile.
14Hatta Yesu alijiofika nyumbani kwa Petro, akamwona mama wa mkewe amelala hawezi homa. 15Akamgusa mkono wake, homa ikamwacha; nae akaondoka, akawatumikia. 16Ilipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo: akawafukuza pepo kwa neno lake, akawaponya wote waliokuwa hawawezi, 17illi litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Mwenyewe alitwaa magonjwa yetu, na kuchukua maradhi zetu.
18Yesu alipoona makutano mengi wakimzunguka, akaamuru kuvuka hatta ngʼambu. 19Mwandishi mmoja akamwendea, akamwambia, Mwalimu, nitakufuata ko kote uendako. 20Yesu akamwambia, Mbweha wana matundu, na ndege za anga vituo; bali Mwana wa Adamu hana pa kulaza kichwa chake. 21Mwingine katika wanafunzi wake akamwambia, Bwana, nipe rukhusa kwanza, niende nikamzike baba yangu. 22Lakini Yesu akamwambia, Nifuate; waache wafu wazike wafu wao. 23Akapanda chomboni, wanafunzi wake wakamfuata. 24Kukawa msukosuko mkuu baharini, hatta chombo kikafunikizwa na mawimbi: nae alikuwa amelala. 25Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwamsha, wakinena, Bwana, tuokoe tunaangamia. 26Akawaambia, Mbona mu waoga, enyi wa imani haba? Marra akaondoka, akazikemea pepo na bahari; kukawa shwari kuu. 27Wale watu wakastaajabu, wakinena. Huyo ni mtu wa namna gani hatta pepo na bahari zamtii?
28Alipofika ngʼambu, katika inchi ya Wagergesene, watu wawili wenye pepo walikutana nae, wanatoka makaburini, wakali mno, hatta mtu asiweze kupita njia ile. 29Wakapiga kelele, wakinena, Tuna nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu? Je, umekuja kutuadhibu kabla ya muhulla? 30Bassi, kulikuwako mbali kundi la nguruwe wengi wakilisha. 31Pepo wakamsihi, wakinena, Ukitufukuza, tuache twende, tukaingie katika kundi la nguruwe. 32Akawaambia. Nendeni. Wakatoka, wakaingia katika kundi la nguruwe: na, kumbe! kundi lote la nguruwe likatelemka kwa kassi gengeni, wakaingia baharini, wakafa majini. 33Wachungaji wakakimbia, wakaenda zao mjini, wakayakhubiri yote, na mambo ya wenye pepo pia. 34Mji wote ukatoka kwenda kumlaki Yesu; walipomwona, wakamsihi aondoke mipakani mwao.

Currently Selected:

Mattayo MT. 8: SWZZB1921

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in