Mattayo MT. 12
12
1WAKATI ule Yesu alipita katika makonde siku ya sabato; wanafunzi wake wakaona njaa, wakaanza kuvunja masuke, wakala. 2Na Mafarisayo walipoona, wakamwambia, Tazama! wanafunzi wako wanatenda lililo haramu kutenda siku ya sabato. 3Akawaambia, Hamkusoma alivyotenda Daud, alipokuwa na njaa, yeye na wenzi wake; 4jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, akaila mikate iliyotolewa kwa Mungu, isiyo halali kuliwa nae wala na wenzi wake, illa na makuhani peke yao? 5Wala hamkusoma katika torati, kwamba siku ya sabato makuhani hekaluni huinajisi sabato wasipate khatiya? 6Lakini nawaambieni, kwamba hapa yupo aliye mkuu kuliko hekalu. 7Kama mngalijua maana ya maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka, hamngaliwalaumu wasio na khatiya. 8Kwa maana Mwana wa Adamu udiye Bwana wa sabato.
9Akaondoka huko, akaiugia katika sunagogi lao. 10Na tazama mtu mwenye mkono umepooza, wakamwuliza, wakinena, Ni halali kuponya watu siku ya sabato? wapate kumshtaki. 11Akawaambia, Ni mtu yupi miongoni mwenu mwenye kondoo mmoja, yule kondoo akatumbukia shimoni siku ya sabato, asiyemshika akamwondosha? 12Je! mtu si hora sana kuliko kondoo? Bassi ni halali kutenda mema siku ya sabato. 13Akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako; akaunyosha, ukapona, nkawa mzima kama mkono wa pili. 14Lakini Mafarisayo wakatoka wakamfanyia shauri la kumwangamiza. 15Nae Yesu akijua haya akatoka huko: makutano mengi wakamfuata; akawaponya wote, 16akawaagiza wasimdhihirishe; 17illi litimie neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema,
18Tazama, mtumishi wangu niiliyemteua;
Mpendwa wangu, ambae moyo wangu umependezwa nae;
Nitamtia roho yangu,
Nae atuwatangazia Mataifa hukumu.
19Hatateta, wala hatapaaza sauti yake;
Wala mtu hatasikia sauti yake njiani.
20Mwanzi uliopondeka hatauvunja,
Wala kitani kitokacho moshi hatakizima,
Hatta aletapo hukumu yake ikashinda.
21Na jina lake Mataifa watalitumainia.
22Wakati ule akaletewa mtu mwenye pepo, kipofu na bubu; akamponya, hatta yule kipofu na bubu akasema na kuona.
23Makutano wote wakashangaa wakasema, Huyu siye mwana wa Daud? 24Lakini Mafarisayo waliposikia, wakasema, Huyu hafukuzi pepo, illa kwa uweza wa Beelzebul mkuu wa pepo. 25Yesu akijua mawazo yao, akawaambia, Killa ufalme ukifitinika na nafsi yake, hufanyika ukiwa; na killa mji au nyumba ikifitinika na nafsi yake, haitasimama. 26Na Shetani akimfukuza Shetani, amefitinika na nafsi yake; bassi ufalme wake utasimamaje? 27Na mimi nikifukuza pepo kwa uweza wa Beelzebul, je! wana wenu wawafukuza kwa uweza wa nani? Kwa sababu hii hawo ndio watakaokuwa waamuzi wenu. 28Lakini mimi nikifukuza pepo kwa uweza wa Bobo ya Mungu, bassi ufalme wa Mungu umekujieni. 29Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? ndipo atakapoiteka nyumba yake. 30Mtu asiye upande wangu yu kinyume changu; na mtu asivekusanya pamoja nami hutapanya. 31Kwa sababu hii nawaambieni, Killa dhambi na killa neno la kufuru watasamehewa wana Adamu, bali kumtukana Roho hawatasamehewa wana Adamu. 32Na killa mtu atakaenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakaenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ntakaokuwa. 33Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri; au ufanyeni mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hujulikana. 34Uzao wa nyoka, mwawezaje kusema mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake.
35Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa mema: na mtu mbaya katika hazina yake mbaya hutoa mabaya, 36Bassi, nawaambieni, Killa neno lisilo maana, watakalolisema wana Adamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu. 37Maana kwa maneno yako utapewa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.
38Hapo baadhi ya waandishi na Mafarisayo wakamjibu, wakinena, Mwalimu, twataka kuona ishara kwako. 39Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zina chataka ishara, wala hakitapewa ishara, ilia ishara ya nabii Yunus. 40Maana kama vile Yunus alivyokuwa siku tatu mchana na nsiku katika tumbo la nyamgumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa inchi. 41Watu wa Ninawi watasimama siku ile ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nao watakihukumu: maana wao walitubu kwa makhubiri ya Yunus; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yunus. 42Malkia wa kusini ataondoka siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nae atakihukumu: maana yeye alikuja kutoka pande za mwisho za ulimwengu asikie hekima ya Sulemani; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani. 43Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupita kati ya pahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate. 44Khalafu hunena, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa. 45Marra huenda, akachukua pamoja nae pepo wengine saba walio waovu kupita nafsi yake, nao huingia na kukaa humo; na mambo, ya mwisho ya mtu yule huwa mabaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kiovu.
46Alipokuwa katika kusema na makutano, mama yake na ndugu zake walikuwa wakisimama nje, wakitaka kusema nae.
47Mtu akamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kusema nawe. 48Akajihu, akamwambia yule aliyempa khabari, Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni nani? 49Akawanyoshea mkono wanafunzi wake, akasema. Tazama, Mama yangu na ndugu zangu! 50Kwa maana ye yote atakaeyafanya mapenzi ya baba yangu aliye mbinguni, huyu ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu.
Currently Selected:
Mattayo MT. 12: SWZZB1921
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.