YouVersion Logo
Search Icon

Wimbo ulio Bora 7

7
Maelezo ya wasifu
1 # Zab 45:13 Binti wa kimalkia, jinsi ulivyo mzuri
Hatua zako katika mitarawanda.
Mapaja yako ya mviringo ni kama johari,
Kazi ya mikono ya fundi stadi;
2Kitovu chako ni kama bakuli la mviringo,
Na isikose divai iliyochanganyika;
Tumbo lako ni mfano wa chungu ya ngano,
Iliyozungukwa na ugo wa nyinyoro;
3 # Wim 4:5 Matiti yako mawili ni kama wanapaa wawili,
Ambao ni mapacha ya paa;
4Shingo yako ni kama huo mnara wa pembe;
Macho yako kama viziwa vya Heshboni,
Karibu na mlango wa Beth-rabi;
Pua yako ni kama mnara wa Lebanoni,
Unaoelekea Dameski;
5Kichwa chako juu yako ni kama Karmeli,
Na nywele za kichwa chako kama urujuani,
Mfalme amenaswa na mashungi yake.
6Jinsi yalivyo mazuri, yalivyo matamu,
Mapenzi katikati ya anasa!
7Kimo chako kimefanana na mtende,
Na matiti yako na vichala.
8Nilisema, Nitapanda huo mtende,
Na kuyashika makuti yake.
Matiti yako na yawe kama vichala vya mzabibu,
Na harufu ya pumzi yako kama mapera;
9Na kinywa chako kama divai iliyo bora,
Kwa mpendwa wangu inashuka taratibu,
Ikitiririka midomoni mwao walalao.
10 # Wim 2:16; Gal 2:20; Zab 45:11 Mimi ni wake mpendwa wangu,
Na shauku yake ni juu yangu.
11Njoo, mpendwa wangu, twende mashambani,
Tufanye maskani katika vijiji.#7:11 Au, penye maua ya mhina.
12 # Wim 6:11; 4:16; Zab 63:3-8; 73:25 Twende mapema hadi mashamba ya mizabibu,
Tuone kama mzabibu umechanua,
Na maua yake yamefunuka;
Kama mikomamanga imetoa maua;
Huko nitakupa upendo wangu.
13 # Mwa 30:14; Wim 5:1; Mt 13:52; Yn 15:8 Mitunguja hutoa harufu yake;
Juu ya milango yetu yako matunda mazuri,
Mapya na ya kale, ya kila namna,
Niliyokuwekea, mpendwa wangu.

Currently Selected:

Wimbo ulio Bora 7: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in