YouVersion Logo
Search Icon

Zaburi 99

99
Sifa kwa utukufu wa Mungu
1 # Kut 25:22 BWANA ametamalaki, mataifa wanatetemeka;
Ameketi juu ya makerubi, nchi inatikisika.
2BWANA ni mkuu katika Sayuni,
Naye ametukuka juu ya mataifa yote.
3 # Kum 28:58; Isa 6:3; Ufu 4:8 Na walisifu jina lake kuu litishalo;
Ndiye mtakatifu.
4 # Kum 32:3,4; Ayu 36:5; Isa 11:3-5; Yer 23:5; Mwa 18:25 Mfalme mkuu#99:4 Katika Kiebrania ni nguvu za mfalme. upendaye hukumu kwa haki;
Umeiimarisha haki;
Umefanya hukumu na haki katika Israeli.
5 # 1 Nya 28:2; Zab 132:7; Isa 66:1 Mtukuzeni BWANA, Mungu wetu;
Sujuduni penye kiti cha miguu yake;
Ndiye mtakatifu.
6Musa na Haruni walikuwa makuhani wake,
Na Samweli pia ni miongoni mwa walioliitia jina lake,
Walimlilia BWANA naye akawaitikia;
7 # Kut 19:9; 33:9; Hes 12:5 Akasema nao katika nguzo ya wingu.
Wakashika shuhuda zake na amri aliyowapa.
8 # Hes 14:20; Sef 3:7; Kum 9:20 Ee BWANA, Mungu wetu, ndiwe uliyewajibu;
Ulikuwa kwao Mungu mwenye kusamehe
Ingawa uliwapatiliza matendo yao.
9Mtukuzeni BWANA, Mungu wetu;
Sujuduni mkiukabili mlima wake mtakatifu;
Maana BWANA, Mungu wetu, ni mtakatifu.

Currently Selected:

Zaburi 99: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in